Picture
Baadhi ya walimu waliojitolea kuwasomesha watoto akiwemo Mratibu wa darasa hilo na pia katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwana Amos Cherehani (Wakwanza kulia) akitoa maelezo juu ya ufunguzi wa darasa la Kiswahili lililofunguliwa rasmi kwaajili ya watoto, Siku ya Jumamosi, tarehe 23 March 2013 Callege Park Maryland Nchini Marekani.
Watoto hao ambao ni wanafunzi wa darasa hilo waliweza kujiandikisha na pia kupangwa kwa makundi kutokana na uelewa wao wa kujua lugha ya Kiswahili na baada ya hapo watoto walijiandikisha na kuazishwa somu la kujua herufi za A,E,I,O,U.


Walimu walijitahidi sana kwa watoto waliojiandikisha na baadae kufundishwa kujua kuongea Kiswahili, chini ya Mratibu Mkuu wa darasa hilo bwana Amos Cherehani na kumkaribisha Mgeni rasmi ambae alikua Rais wa Jumuiya ya waTanzania waishio DMV Bwana Iddi Sandaly.
Picture
Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bwana Iddi Sandaly akiwakabidhi zawadi wanafunzi waliojiandikisha katika darasa hilo.
''Nimefurahishwa  sana na pia  nawashukuru sana wazee pamoja na walimu ambao wameshiriki kwa kujitolea pamoja na wazee kuwaleta watoto wao kwa lengo la kujifunza lugha yetu ya Kiswahili tuko pamoja na tutashirikiana kuendeleza utaratibu huu kwa watoto wetu'', alisema Bwana Iddi Sandaly.


Mpangilio mzima ulioazishwa wakukuza na kuitunza lugha ya kiswahili kwa watoto wa waTanzania wanaoishi DMV  ni kama ajira kwa watoto wetu alisema Mratibu wa darasa hilo bwana Amos Cherehani ambae pia ni Katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV.

Aidha Mratibu Mkuu wa darasa la kiswahili bwana Amos Cherehani aliwaomba waTanzania wanaoishi hapa DMV ambao wamebarikiwa kua na watoto wenye umri wa kwenda shule waje kujiunga na kuwaleta watoto wao kujifunza lugha ya Kiswahili bila ya malipo.
Picture
Baadhi ya watoto wanafunzi waliohudhuria kujiandikisha katika darasa la kiswahili na kuanza kujifunza kiswahili pamoja na kuhamasiswa wazee wajitahidi kuwafundisha kujua vitu tafauti kwa majina ya Kiswahili.Picture
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV Amos Cherehani pamoja na uongozi mzima akihamasisha watoto wanafunzi pamoja na wazee kuhusu umuhimu wa kuongea lugha ya Kiswahili Ughaibuni ni kama ajira alisema Mwenyekiti.

picha na Swahili Villa blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. I really admire wabongo wa Washington. Next thing they have a CCM or Chadema elections etc. It seems to be a very buy town for wabongo.The good thing you are very organised compared to some cities I have been to. Good luck and all the best!!!

    ReplyDelete
  2. Ni hatua ya kupogezwa!

    Pana Mdau mmoja hukoHelsinki Finland wiki ya jana alitushukia humu jamvini akiwa anahitaji msaada mwanawe hajui kuimba kwa lugha ya Kiswahili ktk Sherehe ya siku yake ya kuzaliwa huko Finland.

    ReplyDelete
  3. Muendeleze hadi Utamaduni wa Mtanzania zaidi ya Kiswahili.

    Kwa kuwa Lugha inakwenda na Utamaduni!

    ReplyDelete
  4. Nawaonea huruma watoto wa kitanzania alafu hawajui kiswahili, wazazi jitahidini, sasa kipare, kijaruo, kisukuma.

    ReplyDelete
  5. Kama Mdau wa tatu hapo juu anavyosisitiza Utamaduni na Lugha, inatakiwa ktk mchakato wa masomo hayo ya Kiswahili wanapangiwa siku wanafungwa vibwebwe na kuchezeshwa Midumange na Lizombe ngoma za Makabila ya Kitanzania.

    Yaani itakuwa muruwa sana, kwa Makabila yetu 126 nchini nadhani wakianza ngoma ya Kabila moja watarudia mara 2 tu Kabila hilo kwa mwaka mzima.

    Ni vile mzunguko utawapa kuicheza ngoma ya Kabila moja kwa mara mbili tu kwa mwaka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...