Tunapozungumzia watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na kuviendeleza vipaji hivyo hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la Sensei Rumadha Fundi aka Romi (pichani) hatuwezi kulikwepa. Yeye ni Mtanzania mwenye makazi yake huko Texas, nchini Marekani.
Kabla ya kujikita huko Romi alikuwa moja ya wanafunzi wa karate pale Zanaki jijini Dar es salaam chini ya mwalimu wake Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP), akiwa mmoja wa vijana wadogo wateule wa mwalimu huyo aliyebuni kundi maalumu la vijana hodari wa mchezo huo, kwa jina Bomani Brigade.
Baada ya hapo Sensei Rumadha akaenda kwa mafunzo zaidi huko Okinawa nchini Japan, Sweden na Denmark. Pia akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa mtaalamu wa Yoga.
Kwa vipaji hivi vya Karate na Yoga, Sensei Rumadha Fundi anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji, akiwa ni mwalimu wa karate na yoga mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana na mwenye nidhamu.
Sensei Rumadha ni mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii ughaibuni. Ni matumaini yetu wahusika katika sekta ya michezo hasa upande wa mapambano kama ngumi, kick boxing, judo na kadhalika wataangalia uwezekano wa kupata mchango wao ambao unaweza kusaidia katika kuboresha wanamichezo wetu kufikia kiwango cha kimataifa na kuliletea sifa taifa letu.
Sensei Rumadha Fundi 'Romi' (3rd Dan black belt), akiwajibika katika semina ya karate katika Dojo ya Sugarland, Texas, nchini Marekani katika semina ya walimu wa karate (ma-sensei) chini ya uongozi wake Sensei Ramon Veras (7th Dan), wa Traditional Okinawan Goju Ryu Karate-Do.
Sensei Rumadha ni mtaalam aliyebobea kwani alianza mazoezi akiwa kijana mdogo na tangu wakati huo hajasimama amekuwa akiendelea kujiboresha kwa kufanya mazoezi ya karate kwa miaka mingi kwa hiyo ana uzoefu, ushupavu na ujasiri ulioupata kwa mazoezi ya dhati, pia ni mwalimu mpole mwenye moyo wa kujitolea pamoja na kusaidia watu wengine..... watanzania tutanufaika sana na wataalamu kama Sensei Rumadha fundi!
ReplyDeleteSensei Rumadha anakubalika kimataifa,
ReplyDeleteKarate na Yoga ni mtaalamu anayeweza kuelemisha umma
Ankal,haya ndio mambo,kumbe yule freddy macha sio mwalimu wa Yoga au karate? bali alidandia tu !kumbe watalaamu wenyewe waliobobea katika Yoga na Karate na kutambuiwa kimataifa wapo? Big Up Sensei Rumadha Fundi
ReplyDeletenimekumbuka enzi za gojirawa okinuu enzi zetu palea zanaki sec school michuzi Bernad King dom yuko wapi?
ReplyDeleteSensei Rumadha kifaa cha kazi tena ni fahari ya watanzania kujivunia
ReplyDeleteShemeji yangu huyo, Mnyamwezi kiukweliukweli!
ReplyDelete