Maonyesho ya 20 ya Siku ya Wakulima Tanzania (NaneNane) yameanza rasmi jana Agosti 1 katika viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.Maonyesho hayo ambayo yapo chini ya Udhamini Mkubwa wa TIB Development Bank,yanaendelea kwa kasi mpaka hapo itakapofikia kilele chake Agosti 8,2013.
Sehemu ya Ngoma za asili zikiendelea kutumbuiza katika ugunguzi wa Maonyesho hayo ya 20 ya Siku ya Wakulima Tanzania (NaneNane) yanayoendelea kwenye viwanja Nzuguni mjini Dodoma.
Baadhi ya Wageni na Viongozi wakifatilia Burudani hiyo ya ngoma.
Muonekano wa Jengo la Mdhamini Mkuu wa Maonyesho hayo mwaka huu wa 2013.
Kwa hiyo siku hizi haiitwi tena TIB(TANZANIA DEVPT BANK)? Bali TIB DEVPT BANK LTD......oooh kumbe!
ReplyDeleteDuuuh haya majina ebu tuwe tunayaweka inavostahili maana hata inakuwa haieleweki tunamaanisha nini. Badala ya kumtangaza mdhamini wako unakuwa unamdhalilisha. Nao wadhamini wanatakiwa wahakiki mabanko yanayoenda kwa jamii kabla ya kuwekwa. Inawezekana ni mie tu naona huo mkanganyiko wa jina la hiyo benki.
ReplyDeleteMdau, Benki ya Rasilimali Tanzania (Tanzania Investment Bank) imebadili jina na sasa inajulikana kama Benki ya Maendeleo ya TIB (TIB Development Bank).
ReplyDelete