Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ameshinda nafasi hiyo kwa kura 487 dhidi ya mpinzani wake, Mhe. Hashim Rungwe aliyepaya kura 69 kati ya kura 593 zilizopigwa, na saba kuharibika katika uchaguzi uliofanyika muda mfupi uliopita Bungeni mjini Dodoma. Akitoa Neno la Shukrani mara baada ya kupata nafasi hiyo,Mh. Sitta amewashurukuru Wajumbe wote wa Bunge la Katiba kwa kuweza kumpa nafasi hiyo adhimu. Pia amempongeza mpinzani wake,Mh. Hashim Rungwe kwa kukubali matokeo hayo.
 Wajumbe wakipiga kura 
 Upigaji kura ukiendelea
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimpongeza Mhe. Sitta kwa ushindi wake wa kishindo
Hongera sana sana....anaambiwa mshindi
Mikono ya pongezi yazidi kumiminika
Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba mteule Mhe Samwel John Sitta akitoa neno la shukurani kwa Wajumbe kwa imani waliyoonesha kwake kwa kumchagua kwa kura nyingi kushika nafasi hiyo. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Dodoma.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa


  1. Masahihisho

    Rejea vizuri idadi ya kura alizopata Mheshimiwa Sitta. Katibu ametamka kuwa ni kura 487 na Hashim Rungwe amepata kura 69.

    ReplyDelete
  2. Mungu ni mwaminifu sana anajua umhimu wako kwa Watanzania kwani Tunaamini kabisa utatuwekea historia kwenye nchi yetu nakutakia kazi njema na Mungu atakujalia

    ReplyDelete
  3. HALAFU? What next?
    Are we moving forward or tutarejea kwenye kawaida yetu?
    yes Speed in execution japo we know that CCM is notorious "kufunga Gavana"

    ReplyDelete
  4. mbona kura ya siri imefanyika hapa na wote wameikubali, inashindikanaje kwenye mambo mengine?

    ReplyDelete
  5. si kwa muda miezi miwili tu Spika ? au vipi sioni sababu ya kufanya mambo makubwa na manjonjo kama vile hilo bunge la maisha vile , watanzania tumezidi kuiga wakati mifuko yetu mitupu , wenzetu wenye kufanya madoido mifuko yao imejaa , nchi zao hazina njaa , wala shule mbovu , wala hospitali duni, hawana tatizo la maji wala umeme

    ReplyDelete
  6. Uncle,
    1. Kuna awkward situation hapa!
    Kama 6 kapata 487
    na Rungwe kura 69
    huku garasa ni 7
    kufanya jumla 563
    sasa hizo kura 30 zikowapi basi?

    2. Anywzy, Hongera Ndg. 6

    3. Ili kuepuka kuonekana Serikali inaongoza Constituent Assembly, inabidi Mhe. Rais amwengue Ndg. 6 kutoka Baraza la Mawaziri. Huwezi kujua nini kiko mbele, basi isije kuonekana ni mkono wa Serikali. Huu ni Ushauri kwa tahadhari, na pia ni mantiki tu kwamba a sitting Cabinet Minister shouldn't simultaneously be independent from his appointing authority.

    ReplyDelete
  7. Nina mashaka sana na mtu anaekuwaga na usongo na kazi fulani. Na alinung'unika mno alipoondolewa uspika. Kwani wengine ambao hawajawahi kuwa maspika hawawezi? NINA MASHAKA!!!!!

    ReplyDelete
  8. Congratulation Mr Sitta, one of the fewest politicians I respect.

    ReplyDelete
  9. He is a very genuine guy, probably one of the very few left in CCM

    ReplyDelete
  10. I like it!

    Ahsante sana,

    Mwachieni Mhe. Samuel Sitta hata ktk Bunge la kawaida arudi ktk Kiti chake kama zamani!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...