Katika ulimwengu wa leo neno blog siyo kitu kigeni, leo hii karibu kila mtumiaji wa internet anayo blog yake. Blogu hizi kuna zile zinazotembelewa na watu wengi na kuna zile zinazopata watembeleaji kwa mdondo.

Je umewahi kujiuliza kwanini watu hawatembelei blog yako kama wanavofanya kwa blog fulanifulani? Ingawa kuna sababu nyingi kama umri wa blog, umarufu wa mmiliki wa blog nk lakini kuna kuna vitu ambavyo unaweza kuvifanya na vikakuongezea idadi ya watembeleaji.

Hivyo kwenye makala ya leo tutaangalia ni vitu gani vya msingi kuzingatia ili blog yako ivutie wasomaji wengi zaidi.

 1. Ishi kwenye blogu yako, chagua uelekeo unaokufaa.

Kama umekuwa ukifuatilia tasnia hii ya blogu, utagundua kuwa makala nyingi zinazoandikwa kwenye blogu nyingi za Tanzania huwa zinafanana sana, na hata muelekeo wa hizi blogu huwa ni uleule.

 Ingawa ni jambo la kawaida kwa kila mtu kukimbilia sehemu inayopendwa na wengi (blogu za habari), lakini jinsi unavyokimbilia sehemu yenye watu wengi, ndivyo jinsi unavyongeza ushindani.

Siyo tu ushindanni, bali wengi wamejikuta wakiingia kwenye uelekeo ambao hawaumudu hivyo siku ya mwisho wanajikuta wakikopi na kupaste.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Miye sina glob, lakini nina maoni kidogo juu ya namna ya kuwavutia watu watembelee glob yako. Nakubaliana na unayosema hapo juu. Mimi kwa mfano hutembelea glob ya mjomba takriban mara tatu au zaidi kila siku. WHY
    Kwa sisi tulio ughaibuni ni kama kitovu kinachotuunganisha na Bongo. Kuna habari za nyumbani ambazo hatuzipati kwenye native newspapers huku.
    Kisha kuna nafasi ya kusikia ndugu wenye maoni yaani ni kama ukumbi watu waja wapiga gumzo. Na glob nyingine huzitembelea mara chache kwa wiki maana nyingi ni predictable, nyingi wakopa habari kutoka kwa majirani. I think running a glob is very difficult and requires dedication and commitment. Ukikutana na mjomba wetu mpe hongera.

    ReplyDelete
  2. kuwa na blog katika fani inayopendwa na wengi ni sawa lakini kinachoniudhi mimi na blog nyingi za tanzania ni kuwa zina habari sawia yaani neno kwa neno. Yaani ukisoma habari moja katika blog moja basi hakuna haja hata ya kusoma nyengine kwani wote wanatumia mfumo wa copy and paste kw kila kitu.

    ReplyDelete
  3. sitaki kusema meni hapa ila ningelitaka kuuuliza kama wengi wetu tumegundua kuwa kuna blog nyingi za vijana wa kitanzania zinazolenga kwenye udaku na uzinifu? nimefanya utafiti mdogo wa kutafuta maneno ya kiswahili katika google na mara nyingi page zinazokuja ni za udaku, uzinifu na video za walijipiga vijana wakifanya mambo yao. Google search maneno video, wanafunzi, bongo, bongo flava na mengine kama haya ndio yanayokithiri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...