Ndugu zangu,

LEO ni Septemba 19, ni Siku ya Kuzaliwa Mtandao wa Mjengwablog.

Kwa mwanadamu, hakupaswi kuwapo na ukomo wa kujitahidi kufanya yalo mema kwa jamii yako.

Na katika kujitahidi kuyafanya yalo mema, basi, mwanadamu uwe tayari kukumbana na changamoto nyingi. Na kama ilivyo kwa maji ya mto, yanapokutana na mwamba, basi, kasi yake huongezeka maradufu.

Leo blogu yako hii ya Mjengwablog imetimiza miaka minane. Miaka minane si haba. Kwa mtoto, aweza kuwa darasa la Pili. Na kwetu wa Mjengwablog ni miaka minane ya kujifunza, kukosea, kujifunza kutokana na makosa, na kisha kusonga mbele.

Kwa niaba ya timu nzima ya Mjengwablog nachukua fursa hii kuwashukuru, kwanza kabisa, mke wangu mpenzi, Mia, ambaye, bila yeye, kazi hii yangu ya kuitumikia jamii ingelikuwa ngumu sana. Pili, niwashukuru kwa dhati wanangu wanne, Olle, John, Manfred na Gustav. Wanawangu hawa wamekuwa na mchango mkubwa pia, ikiwamo kufanya utani na mimi baba yao, ilimradi niwe na wakati wa kucheka, hata pale nilipoona kazi ni ngumu na kukutana na vikwazo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hizi nyumba tunahitaji tuzipige vita kwa sababu hazina ubora bali ni sura ya umasikini uliokaribia kukithiri. Wapalestina wana changisha pesa za kujenga miji yao baada ya miaka mitatu utaona Gaza utakuwa mji baada ya vita. tusiponuia kuziondoa nyumba duni zitaendelea kuwepo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...