Mmiliki wa Jossekazi Auto garage ambao ndiyo waandaaji wa tamasha akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa jina la Automobile Clinic, ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili Septemba 27 na 28, 2014 katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam. Ambapo alisema kuwa tamasha hilo limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa makenika katika aina tofauti tofauti za magari. Pembeni kulia ni Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo na Mwakilishi toka Mwambi Lube Distributor, Jonathan Mwanayongo.

Na Mwandishi Wetu. 

Kampuni ya Jast Tanzania Limited kwa kushirikiana na Jossekazi Auto Garage and General supplier wameandaa tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa jina la Automobile Clinic, ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam. Tamasha hilo limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa makenika katika aina tofauti tofauti za magari.

Akizungumza na vyombo vya habari, kwenye ukumbi wa habari Maelezo, Joseph Mgaya mmiliki wa Jossekazi Auto garage amesema tamasha hili lina lengo kuwakutanisha mafundi stadi na wenye magari, kwa gharama nafuu sana ya shillingi elfu ishirini tu.
Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo akielezea machache juu ya tamasha hilo.

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...