Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akitoa nasaha fupi katika hafla fupi ya kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza ambao wamestaafu rasmi Utumishi wa Umma tangu Julai 1, 2014. Hafla hiyo imefanyika leo Septemba 19, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Wastaafu wa Jeshi la Magereza(katika picha) wakiwa na familia zao wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akitoa nasaha fupi kwa Wastaafu hao ambao wamestaafu Utumishi wa Umma tangu Julai 1, 2014.
Kwaya ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza inayoundwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza ikitumbuiza kwenye hafla hiyo ya kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza. Hafla hiyo imefanyika leo mchana Septemba 19, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishangilia Wimbo Maalum uliotumbuizwa na kwaya ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika hafla fupi ya kuwaaga Maafisa na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza ambao wamestaafu Utumishi wao kwa mujibu wa Sheria tangu Julai 1, 2014.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kulia) akikabidhi zawadi kwa Sajin Taji wa Jeshi la Magereza, Kessy Ngwengwe(kushoto) ambaye alikuwa ni Dreva wa Magari ya Viongozi Makao Makuu ya Jeshi Magereza. Askari huyo amestaafu Utumishi wake wa Umma tangu Julai 1, 2014.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wastaafu wa Jeshi la Magereza(waliosimama mstari wa nyuma) kwenye hafla fupi ya kuwaaga Wastaafu hao ambao amestaafu Utumishi wao wa Umma tangu Julai 1, 2014(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...