SAM_2053
Meneja masoko wa benki ya CBA Tanzania Solomon Kawishe kushoto,Meneja masoko Moshi Eliud Marko katikati wakimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kifaru Abdallah Mwomboke iliyopo katika kijiji cha kituri kata ya kileo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro hundi ya shilingi Milioni tano yenye thamani ya zaidi ya mifuko 300 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika shule hiyo ,msaada huo ni sehemu ya kamapeni ya Book by Book inayoendeshwa na benki ya CBA ikilenga kusaidia serikali katika juhudi za Elimu(Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog)
SAM_2042
Meneja masoko wa Benki ya CBA Tanzania Solomon Kawishe akizungumza na wanafunzi(hawapo pichani) kuhusu nia yao ya kuwasaidia msaada huo wa saruji kwaajili ya kujenga hosteli ni kutokana na idadi ya wanafunzi 944 kuwa na changamoto kubwa ya ufaulu hasa jinsia ya kike huku akiwaasa wanafunzi hao kuwa Elimu ndio urithi pekee wa kuweza kuharakisha maendeleo Tanzania hivyo jamii inategemea kupata watu muhimu wakuwasaidia kama madaktari,wafanyakazi wa mabenki na hata walimu wa kuendeleza elimu
SAM_2038
Meneja masoko Moshi Eliud Marko akiwa anasisitiza wadau mbalimbali wa makampuni makubwa kujitokeza kusaidia kuinua Elimu ili kupunguza umaskini Nchini
SAM_2033
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kifaru Abdallah Mwomboke iliyopo katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro akiwa anatoa neno lake la  shukrani kwa Benki ya CBA kwa kufika na kuguswa kusaidia hosteli ya wasichana katika shule hiyo kutokana na wengi wameshindwa kuendelea na masomo shuleni baada ya kuingizwa katika mahusiano na wanaume hali ambayo inawawia vingumu kuweza kumudu masomo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...