Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam ukiwa umebeba Kaulimbiu isemayo "Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025".
Mhe. Rais Kikwete akizungumza huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakimsikiliza.
Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani).
Wajumbe wengine wakiwemo Wakuu wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete ambaye haonekani pichani.Picha na Reginald Philip.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2015

    Hongera sana Rais kwa kuaga mapema. Wakati ukiwaaga mabalozi ngoja tukumbushana mambo muhimu.
    Rais ajaye atueleze atawezaje kukuza uchumi bila kuendelea kukopa zaidi. Maana msemo wa bado tunakopesheka utatufanya tuwe kama ugiriki. Tusisubiri kufika huko. Tuchukue hatua mapema. Rais ajaye atueleze atalipaje madeni, hiyo ela ataipata wapi na kwa njia zipi. Atakusanyaje kodi. Ataongezaje vyanzo vya kodi. Kama anasema atakuza uchumi na kusomesha watu bure hiyo ela ataipata wapi? Waheshimiwa nawatakia utumishi uliotukuka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...