Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia (pichani kati) akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe,Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba na wa pili kulia ni Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi.Katika mkutano huo ulizungumzia pia kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko  kuungana kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP.
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa UKAWA,uliofanyika mapema leo jijini Dar
  Mmoja wa Wahariri wa gazeti la Jamhuri,Deodatusi Balile akitaka ufafanusi kuhusiana na umoja huo wa UKAWA kumkaribisha rasmi Mhe.Lowassa kujiunga na UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar
 Mmoja wa waandishi mahiri kutoka gazeti la Raia Tanzania,Hafidhi Kidogo aikuliza swali kwa viongozi hao wa UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari na umoja huo,uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar.
 Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama hicho jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wa wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),ambapo mkutano huo ulizungumzia pia kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko  kuungana  kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,kulia ni Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia na kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe pamoja na Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi (hayupo pichani)
  Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama cha CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya kujiunga na UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi wa nane (wiki ijayo) tutamtangaza  mgombea  wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa tumeishapiga hatua ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano huo na Wanahabari.
   Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana makao makuu ya chama cha CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya kujiunga na UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi wa nane (wiki ijayo) tutamtangaza  mgombea  wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa tumeishapiga hatua ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano huo na Wanahabari.
 Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akipeana mkono na Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe mara baada ya kuzungumza na Waaandishi wa Habari  makao makuu ya chama cha CUF,mapema leo mchana jijini Dar,ambapo kwa pamoja kama UKAWA wamemkaribisha rasmi Mhe.Lowassa kujiunga na umoja huo na kwamba watampa nafasi.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
UMOJA wa  katiba ya Wananchi  nchini (UKAWA) vinamkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga katika  na umoja huo pamoja na watanzania wengine katika mapambano ya kuindoa CCM madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Chama cha Wananchi (CUF), kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja huo,Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema wanawalika watanzania wote kujiunga na UKAWA katika kuweza kuleta mabadiliko katika kuhakikisha wanakiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM)  katika kuweza kusimamia nchi.

Mbatia amesema kuwa wanamualika Waziri Mkuu  Mstaafu,Edward Lowassa kutokana na kuwa mchapakazi na mfuatilialiaji katika majukumu ambayo anayatoa na uwezo anao katika kusimamia.Amesema  akiingia Lowassa katika umoja huo watashirikiana kwa karibu kutokana na kutambua kuwa ni mhamasishaji  na  ni mtu mwenye kuthubutu.

Aidha amesema kuwa watamsimamisha mgombea  mmoja katika kila nafasi kupeperusha bendera  ya UKAWA katika uchuguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka  huu.

Nae Mwenyekiti wa Chama Cha  Wananchi (CUF),Profesa Ibrahimu Lipumba amesema tuhuma za ufisadi zinazomkabili Lowassa zinatokana na mfumo  uliopo. Amesema  wanatarajia kutaja jina la mgombea Urais Agosti Nne Mwaka  huu  na atapatikana kutokana na taraibu zilizowekwa na umoja huo.

Mbatia hakuweza kuweka wazi kuwa wanamkaribisha Lowassa kujiunga na chama kipi kutokana na ukawa sio chama kilichosajiliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini.

Mwenyekiti wa NLD,Dk.Emmanuel Makaidi amesema Lowassa akigombea Urais atamkubali na tuhuma zinazomkabili kiongozi zingekuwa za kweli angepelekwa mahakamani lakini bado yupo na wenye tuhuma wamefikishwa mahakamani .

Katika mkutano wa UKAWA masuali yalilenga kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga huko na  tuhuma zake wakati vyama hivyo vilikuwa vikinadi juu ya kutokuwa na usafi na pamoja na uhusikaji katika tuhuma ya mchakato wa  umeme wa dharula kupitia kampuni ya Richmond.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2015

    Huu ni upuuzi mtupu wa Wapinzani. Mimi si mwana CCM na ningependa iondoke lakini kitendo cha wapinzani waliokuwa wana mshambulia Lowassa kuwa ni mwizi na mla rushwa leo kwa njaa yao kali kuingia madarakani wanaona Lowassa ndiyo daraja. Hii inaonyesha jinsi gani upinzani ulivyo dhaifu na kwamba kwa miaka yote hii hamja jiandaa. Nina wasiwasi kama Lowassa atajiunga na UKAWA na hata kama akijiunga bado siyo ticket ya kushinda. Mnajua wazi CCM itafanya kila iwezalo ibakie madarakani na Lowassa analijiua hilo vizuri sana. Achane kutapatapa fanyeni siasa za kujiamani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2015

    Mwembe Yanga, 2007.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2015

    heheheheee ukiona mtu anang'angania kwenda ikulu kwa njia yeyote huyo MUOGOPE kama ukoma.

    Lowasa anataka kurudisha fadhila za walio mfadhili ktk kampeni...Hakuna kujisafisha wala nini...Kina ROSTAM wapo nyuma yake wanategemea malipo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2015

    aogopwe kama ukoma ili iwejee? angekuwa ni babako ungeongea upuuzi huu wacha hizo wee mdau october lazima pachimbikeee come rain come sun! ni ndoto zake tuu anataka azitimeze, ni bora ajaribu akishindwa kihalali ni poa zaidi manake jina lilikatwa wakati mtu ana hamu ya kujaribu halafu unachinjiwa baharini ngoja ajaribu sanduku la kura likigoma hapo roho yake itapoa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 28, 2015

    Moja ya mambo yaliyoipa CHADEMA heshima ni uthubutu na uhodari wao wa kukemea machafu bila kujali hatari na madhara ya kuweka wazi mifumo ya Kimafia nchini. inawezekana Lowassa ni msafi, lakini najaribu kufikiri kwamba CDM hawasikii hata harufu ya uchafu wa Lowassa...yaani hata harufu?!!!.kama kutumika kwa Lowassa sasa kutapambanuliwa na UKAWA kuingia Ikulu, je bado watashikilia Ajenda ya Ufisadi?, kama jibu ni hapana, je Heshima yao itaendelea kuwepo?, kama jibu ni ndiyo, je watamuangaliaje Rais wao?.NI DHAHIRI KUWA SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU,LAKINI MUNGU KWA MAANA YA MUNGU SI JINA BALI NI CHEO CHA MUNGU.MUNGU WA DUNIA HII NI SHETANI,INASIKITISHA WATANZANIA BADO HATUJAJUA KAMA SAUTI HII YA SASA YA WENGI NI YA MUNGU SHETANI AU YA MUNGU MUUMBAJI.NADHANI TUKIYAJUA MAFUNDISHO YA MUNGU MUUMBAJI TATAJUA SAUTI HII NI YA MUNGU GANI.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 28, 2015

    Ukawa wamekosea sana kumkaribisha Lowassa ndani ya chama chao. Lowassa ana uchu wa madaraka, anataka urais by hooks and crooks, atafanya kila aliwezalo apate urais, hii inasikitisha kwa maana hatapata na sijui hali yake ya pili itakuwa mbaya kuliko ya kwanza. Maana wametufanya watanzania kama wajinga, na hatufahamu siasa.
    kila chama kina imani yake, kama vile madhehebu, watu wanaamini suala ambalo kile chama kinakipigania ndio maana wanajiunga, na kile chama kikiona kuna mtu anayefaa kukiongoza kuliko wewe, huhamii chama kingine, unamuunga mkono aliyechaguliwa na kisha unawaisidiana na wanachama wenu kufikisha malengo yenu, mfano wa marekani kwenye uchaguzi uliopita wa Obama, Mrs Clinton alishindwa na Obama, hakuhama chama, alibaki na sasa anagombea tena after 8 years, akabaki kwenye chama na kumshauri aliyechaguliwa, huo ndio ustaarabu.
    Lowassa kuhamia chama kingine, ina maana kwamba, aidha alikuwepo tu CCM wala hakuwa anazijali siasa zake, na alikuwa kwa maslahi yake binafsi. AU anasemaje bado anajali siasa za CCM ila ameenda UKAWA kuwaharibia? au ghafla amependa sera za chadema, it real does not make any sense.
    Kila la heri Lowassa, kwenye sera na dira mpya aidhe unazijua au huzijui, ila mark my word, huji kuwa rais wa Tanzania, and be prepared emotional hilo litakapotokea, sijui utarudi CCM au wapi, muulize mrema
    All the best Tanzania

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 28, 2015

    itabidi UKAWA wamsaidie LOWASSA kujibu swali la Baba wa Taifa hayati, J.K. Nyerere juu ya uhalali wa mali alizonazo....... kweli njaa humfanya mtu ale matapishi yake..... mwanzo, upinzani mlimshambulia LOWASSA kuwa ni fisadi (yalitamkwa na Mbowe na wana Chadema), Mla rushwa (yalitamkwa na Mbatia na NCCR) mmoja wa Mapapa wa rushwa Tanzania (yalitamkwa na Lipumba) then leo ooo ni mfumo wa CCM ndiyo unaoruhusu rushwa na ufisadi.... upinzani achene uongo na mkubali kuwa nyinyi siyo 'visionaries' na ni njaa tuu mliyonayo... hamna lolote

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 28, 2015

    Hamna upinzan Tz ukitaka kujua hilo bora ibaki ccm mana hao wapinzani ni wezi na hawajifahamu haiwezekani wakamleta mtu walokuwa wanamtuhumu.Kama walidai hafai vipi leo awafae??????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...