Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na wanao kwenda kupeperusha bendera ya benki hiyo pamoja na bendera ya CCBRT katika kilele cha mlima wa Kilimanjaro ikiwa ni kukamilisha mchango wao kama benki kwaajili ya watoto waliozaliwa ikiwa miguu yao imepoza ili wapatiwe matibabu katika Hospitali ya CCBRT, ikiwa ni mchango wao kama benki kusaidia jamii inayosumbuliwa na ugonjwa wa kupinda miguu unaojulikana kwa jina la (KIBWIKO) benki ya BOA imekusanya kiasi cha dola 100,000  kwaajili ya kuchangia matibabu ya wanaopatwa na matatizo hayo, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo.
 Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi  akimkabidhi bendera ya Hospitali ya CCBRT Mwenyekiti wa wafanyakazi wa benki ya BOA, Bruno Ngooh leo jijini Dar es Salaam, ambapo itatia moyo kwa makampuni binafsi kuchangia jamii kama walibyofanya benki hiyo.
Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi  akimkabidhi bendera yenye nembo ya BOA benki  pamoja na nembo ya Hospitali ya CCBRT Mwenyekiti wa msafara wa wafanyakazi wa benki ya BOA, Bruno Ngooh leo jijini Dar es Salaam,ikiwa Mkurugenzi huyo akiwatakia kila raheri wafanyakazi wa benki hiyo kufanikiwa kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro na kurudi wakiwa na kumbukumbu kwao pamoja na ushindi katika jamii ikiwa ni faida na hata kwenye afya zao kwa ujumla alisema.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...