Na Shamimu Nyaki-Maelezo

Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limewakamata wahamiaji haramu 105 raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa wanasafirishwa kwenda nchi nyingine za Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaamu Kamishna Suleiman Kova amesema wahamiaji hao ambao wote ni wanaume wamekamatwa kutokana na ushirikiano wa wasamaria wema wanaoshi eneo hilo la Tabata Segerea.

Ameongeza kuwa wahamiaji hao waliingia nchini ya usimamizi wa mwanamke mmoja anaeitwa Zainabu Umwiza (25) anaesemekana ni raia wa nchi ya Burundi ambae anajihusisha na biashara hiyo ya usafirishaji haramu wa binadamu ambao ni kosa la jinai tayari kuwapeleka nchi nyingine na hivyo amemuomba ajisalimishe
“ Bi Zainabu Umwiza mwenye asili ya Burundi tunamwomba ajisalimishe maana yeye ni mfanyabiashara wa usafirishaji wa binaadamu  kutoka nchi za Afrika kwenda Ulaya” kamanda Kova alisisitiza.

Aidha kamanda Kova ameeleza kuwa polisi walifanya upekuzi katika nyumba ya mwanamke huyo ndipo walipowakuta wahamiaji hao ambapo uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, usafirishaji wa binadamu kutoka Afrika kwenda bara la Ulaya unaofanywa na mwanamke huyo, ambao hufanyika kwa malipo ya Dolla 1000 kwa mtu mmoja.

Kamanda Kova ameongeza kuwa watuhumiwa hao walipohojiwa kujua kwamba wana kibali chochote cha kuingia nchini waligunduliwa kuwa hawana na kueleza kuwa waliingia kupitia njia za panya na mbinu nyingine ambazo bado zinachunguzwa na kwamba wamewajulisha  idara ya Uhamiaji na watashirikiana nao katika upelelezi ili hatimaye sheria ichukue mkondo wake.

Hata hivyo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kundoa na kuzuia tatizo la wahamiaji haramu ambao wamekua tishio katika usalama wa maisha ya wananchi na mali zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...