Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM) kwa Tanzania unatoa tena wito kwa ukamilishwaji haraka wa mchakato wa uchaguzi Zanzibar kulingana na kanuni za chaguzi shirikishi, za uwazi, zinazotekelezwa kwa wakati na za kuaminika. 

Kufuatia Siku ya Uchaguzi tarehe 25 Oktoba, Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya umebaki nchini kufuatilia chaguzi zilizoahirishwa Tanzania Bara na mchakato uliyositishwa Visiwani Zanzibar, baada ya tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) la tarehe 28 Oktoba, lililofuta matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar.

 EU EOM ilikutana na wadau wakuu Visiwani, vikiwemo vyama vya siasa, Mwana Sheria Mkuu wa Serikali wa zamani na wa sasa, wadau wa sharia na mahakama, asasi za kiraia na maafisa uchaguzi. Bahati mbaya EU EOM haikuweza kukutana na Mwenyekiti wa ZEC.

EU EOM inafahamu kuhusu mazungumzo yanayoendelea kati ya CCM na CUF, yanayowashirikisha Marais Wastaafu wa Zanzibar. EU EOM inarudia tena wito uliyotolewa kwa pamoja na jumbe zingine za uangalizi za kimataifa tarehe 29 Oktoba, unaoishauri ZEC kuonyesha uwazi kamili kufuatia uamuzi wake wa kufuta uchaguzi na uongozi wa kisiasa Zanzibar kuweka maslahi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar kwanza, kwa lengo la ukamilishwaji haraka wa mchakato wa uchaguzi, kulingana na kanuni za kidemokrasia za chaguzi pamoja na sheria za Zanzibar.

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hawa eu wakae mbali na sisi. hawana kazi bali kutafuta umbea kula fedha ya wananchi wao kuwa eti wanasambaza demokrasia. yamewashinda misri sasa wanatafuta pa kujipatia umaarufu. demokrasia yao sio lazima iwe yetu. tusikubali kurubuniwa na wahuni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...