TAMASHA la Pasaka 2016 linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions jijini Dar es Salaam linatarajia kufanyika Machi 27 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama mkoa wa Mwanza umepata bahati hiyo baada ya wakazi wake kuomba kwa kipindi kirefu kufikiwa na tamasha hilo.

“Kamati yangu huwa inasikia matakwa ya mashabiki wa muziki wa Injili kwa sababu tamasha hilo ni lao ni vizuri kuwasikiliza,” alisema Msama.Msama alisema, Kamati yake imekaa na imechunguza Tamasha la mwaka huu lifanyikie jijini humo, hivyo anatoa wito kwa wakazi wa jiji hilo kujiandaa vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo.

“Tamasha letu linawahusu wenye uhitaji maalum ambao ni walemavu, wajane na yatima ambao misaada yao inatokana na tamasha hilo, hivyo wajipange na kujitokeza kwa wingi,” alisema Msama.

Msama alisema wamesikia kilio cha Wananchi Mwanza baada ya maombi yao ya muda mrefu, tamasha litafanyikia jijini humo ikiwa ni heshima yao.“Wakazi wa Mwanza walipokee, waimbaji mbalimbali wa mataifa mbalimbali, ni sherehje, raha, vifijo,” alisema Msama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...