Katika kudumisha urafiki mwema  kati ya  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  (JKCI)  na Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi amefanya ziara kutembelea hospitali hiyo na kuonana na madaktari bingwa wa moyo pamoja na watoto wa Kitanzania kadhaa waliopewa rufaa kwenda kupata matibabu hapo.
Profesa Janabi ameiambia Globu ya Jamii kwa njia ya simu kutoka Tel Aviv kuwa Serikali ya Israel kupitia mpango wake wa Save a Child's Heart  (Okoa moyo wa mtoto) ni moja ya washirika wakubwa wa JKCA katika kubadilishana utaalamu na vifaa.
 “Washirika wetu wengine ni Open Heart international ya Australia, Mending Kids Heart ya California, Madaktari Africa ya South Carolina, Almutada ya Saudi Arabia, Sharjah International ya UAE na Madras Medical mission and BLK  ya India.
“Hawa wote kwa muda mbalimbali huw wanakuja JKCI na mpaka sasa  katika mwaka huu wa 2016 wamekuja BLK, Madaktari Africa na lsrael” alisema, na kuongezea kuwa “Kwenye hospital ya moyo ya Wolfson tunayoshirikiana nayo JKCI. Nimeona watoto wetu 11 tuliowaleta huku wakiwa na complicated cases. Tisa wamekwisha fanyiwa upasuaji bado wawili na wote wanatokea Zanzibar.
Profesa Janabi ameongozana na manesi watatu na daktari mmoja.

  Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi baadhi ya wenyeji wake katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
 Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi akiwa na madaktari bingwa wa moyo katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
 Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi akiongea na Mkuu wa Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
 Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi akiwa ametoka kusaidia upasuaji na madaktari bingwa wa moyo katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi akiwa na baadhi ya wagonjwa na walezi wao waliofanyiwa upasuaji  katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake. Bango aliloshika linaonesha majina ya wagonjwa kutoka Tanzania waliofanyiwa upasuaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mungu akubariki kwenye majukumu yako profesa. unaonekana wazi ni mtu muhimu sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...