KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, imefanya ziara ya kutembelea mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal Three- TBIII), jijini Dar es Salaam, Machi 29, 2016 ambapo awali wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Profesa Norman Adamson Sigalla King, walipatiwa maelezo ya kina ya maendeleo ya mradi huo unaohusisha jengo la kisasa la abiria na sehemu ya kuegesha ndege kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na sehemu ya maegesho ya magari. Baada ya maelezo hayo ya kina yaliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, (TAA), Mhandisi George Sambali akisaidiana na baadhi ya wakurugenzi wengine wa Mamlaka hiyo, wajumbe hao walitembelea mradi huo na kujionea hatua mbalimbali za ujenzi ambapo kwa sasa ujenzi umefikia karibu asilimia 60. Pichani, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali, (kushoto), akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Norman Adamson Sigalla King, (kulia), na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA.
 Mwenyekiti wa Kamati, akizungumza
 Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha, akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge kabla ya kutembelea mradi
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo na maafisa wa TAA, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali (hayupo pichani)
 Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga, (kulia), akitoa maelezo ya maeneleo ya mradi huo. (kushoto) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA, Laurent Mwigune.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Habari ingenoga zaidi kama picha la jengo jipya la uwanja wa ndege linaojengwa ingewekwa kama kama ndo ''kichwa cha habari'' hapa globu ya jamii badala ya ''kuuza sura za waheshimiwa wana kamati a.k.a wabunge wakati picha ya mradi unaokaguliwa kufichwa ktk '' bofyaa hapa kwa picha zaidi.

    Mdau Mkongwe
    Globu ya Jamaii

    ReplyDelete
  2. mdau bofya kitufe hapo chini utayaona mapicha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...