Na Bashir Yakub.
Kazi kubwa ya sheria zote zinazoshughulika na masuala ya ardhi ni kuratibu na kutoa mwongozo katika miamala mbalimbali ya masuala ya ardhi katika maisha ya kila siku.
Miamala hiyo ni kama uuzaji na ununuzi wa ardhi, masuala ya mikopo na rehani, upangaji na upangishaji, masuala ya fidia, kuhamisha umiliki, haki na wajibu wa mmiliki ardhi, haki na wajibu wa serikali katika ardhi yote, upimaji na ramani, namna ya kutatua migogoro ya ardhi, n.k.
Makala yatagusa kwa mtindo wa dondoo baadhi ya mambo ya msingi yaliyo katika sheria ya ardhi namba 4 ya 1999 sura ya 113.
1.SHERIA NAMBA 4 YA MWAKA 1999.
Sheria hii ilipitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano mwaka 1999. Hata hivyo ilianza kutumika rasmi mwezi mei mwaka 2001.
( a ) MDHAMINI WA ARDHI YOTE NI RAIS.
Sehemu ya pili ya kifungu cha 3 cha sheria hii inaanza kwa kueleza sera ya taifa ya ardhi. Kubwa linalotajwa ni kuwa ardhi yote ni mali ya umma ambayo mdhamini wake ni rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania. Huu ndio msingi mkuu wa ardhi yetu.
( b ) WASIMAMIZI WAKUU WA ARDHI.
Sehemu ya iv kifungu cha 8 mpaka 18 kinaeleza watumishi wakuu na wasimamizi wa ardhi kitaifa. Waziri wa ardhi ndiye mwenye dhamana kuu akifuatiwa na kamishna mkuu wa ardhi kabla ya kutajwa kamishna msaidizi na baadae maafisa ardhi . Wajibu, kazi na majukumu yao yameainishwa katika vifungu hivyo. Sambamba na hilo mipaka katika utekelezaji wa majukumu yao ni jambo jingine lililoainishwa.
( c ) KUMILIKI HATI.
Sehemu ya vi kifungu cha 24 mpaka 30 yameelezwa masuala ya hakimiliki. Taratibu za kupata hakimiliki na umilikishwaji . Wakati huohuo vifungu vya 31 mpaka 35 vimeeleza vyema masharti yanayoambatana na hakimiliki ,muda wa hakimiliki pamoja na kodi za ardhi.
Kifungu cha 76 mpaka 78 kimeongelea uuzaji wa ardhi hasa zenye hati miliki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...