Rais Dkt Magufuli akizungumza na Uongozi wa juuu wa Benki Kuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kweli yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Pongezi za dhati kwa Mh. Rais wetu JPM. Naamini Mh. Rais wetu, kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wetu wa awamu hii ya tano, kayashuhudia mengi yaliyokuwa yakitendeka ndivyo sivyo, lakini ndio hivyo pengine kwa namna moja ama nyingine, hayakuwa ndani ya uwezo wake kuyakemea, kuyaingilia kati au hata kuyatafutia suluhu ya aina yeyote ile, naamini alikuwa akiona uchungu sana kwa mambo yalivyokuwa yakiendeshwa mbele nyuma, ndivyo sivyo. Lakini sasa hivi kweli imedhihiri, hakuna tena zile nadharia hewa zisizokuwa na vitendo, ufatiliaji wala majibu. Kweli Tanzania siyo Shamba la bibi tena.

    Mungu ibariki Tanzania na Raia wake, Ibariki Afrika na Dunia kwa jumla.

    ReplyDelete
  2. The mdudu, yaani mimi nashindwa kuelewa hivi sisi watanzania tuna matatizo gani kwenye vichwa vyetu mbona wafanyakazi wa hiyo Bank nyeti ya nchi yetu wanaonekana wapo wapo tu hawajui walifanyaro si rais wetu Magufuli alivamiaga hapo na alikuta madudu na bado yanaendelea? huku sasa ni kucheza na maisha ya watanzania ndugu zangu kama kazi hamuezi mjitoe wenyewe ili wanaojua kuchapa kazi waingie hapo na wewe waziri chukua mfano wa uchapakazi wa rais wetu sasa jamani hivi ni nini maana ya uongozi?

    ReplyDelete
  3. Asante Baba nchi ilikuwa imeoza. Kila mtu hajali ni kula, kula, kula kula, kula, kula, kwa saizi ya mdomo wake. Wote hao hawaoni wala kuamini yote unayoyafanya, hawaamini! wao wanaona kama wewe uko usingizini na wao ndiyo wako macho!!
    Tusaidie.Na Mwenyezi Mungu awe nawe, mishale yao iwarudie wenyewe.
    HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  4. Ahsante Raisi wetu ,Tunamwomba Mungu akulinde na akupe hekima na busara kufanya kazi yako ,Tanzania tuipendayo na yenye maendeleo inakuja.
    Kwenye sector nyeti kama hizi za serikali panatakiwa kuwepo kwa Payrol analyst kukagua na kuhakiki ulipaji wa mishahara

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...