Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke walioko masomoni na likizo wametakiwa kurudi mara moja katika vituo vyao vya kazi ili kuhakikiwa.

Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na uongozi wa Halmashauri hiyo ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli la kuhakiki watumishi wote wa umma waliopo kwenye orodha ya malipo ya watumishi wa umma ndani ya siku 15 ili kubaini watumishi hewa wanaoendelea kulipwa mishahara.

Akizungumza kwa njia ya simu msemaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Bi Joyce Nsumba amesema zoezi hilo ni muhimu sana kwa watumishi hivyo basi  watumishi wote wa Halmasahuri hiyo waliopo likizo na masomoni wanatakiwa kurudi katika vituo vyao vya kazi ili kuhakikiwa.

“ Taarifa imeshatoka kwa watumishi wote kuwa wanatakiwa kuhakikiwa na kwa wale waliopo likizo na kwenye masomo wanatakiwa kurudi ili wahakikiwe na kuendelea na likizo na masomo yao kwani mara baada ya uhakiki huu kukamili majina ambayo yatakuwa hayajahakikiwa yatafutwa kwenye orodha ya  watumishi” Alisema Bi Joyce.

Bi Joyce Nsumba ameongeza kuwa mpaka sasa uhakiki unaendelea  kwa makundi mbalimbali wakiwemo watumishi kutoka Idara ya Afya, Elimu, Fedha na Biashara, Kilimo,Mifugo,Ujenzi,na Maendeleo ya Jamii na mpaka  sasa wameshahakiki zaidi ya watumishi  8,000.

Zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma nchini limekuja mara baada ya uchunguzi uliofanywa katika mikoa ya Singida na Dodoma katika Halmashauri 14 na kugundulika kwa watumishi hewa 202 wanaolipwa mishahara  na hivyo Mhe. Rais Magufuli kutoa agizo la kuhakiki watumishi wote katika Wizara,mikoa,Wilaya,Idara,Taasisi na Wakala za Serikali ndani ya siku 15.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...