Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akizungumza jana katika Mkutano wa nane wa wadau wa LAPF unaoendelea jijini Arusha katika ukumbi wa AICC ambapo alikuwa mgeni rasmi mbali na mambo mengine,aliitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa mafao kwa wakati pindi wanachama wake wanapostaafu ili kuhakikisha kuwa wastaafu wanapata mafao yao, kwani wengi wao wanakabiliwa na msongo wa mawazo kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili baada ya kustaafu wanashindwa kujimudu kutokana na kukosa mafao yao(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha).

Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge ,Ajira na Walemavu Jenister Mhagama ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye viwanda ili kuunga mkono msimamo wa serikali kuanzisha uchumi wa viwanda utakaotengeneza ajira na kuchochea maendeleo ya nchi

Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF Eliudi Sanga akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kuwa Mifuko ya hifadhi ya jamii imekua chachu ya maendeleo ya taifa kutokana na uwekezaji unaofanywa na mifuko hiyo pamoja na mikopo mbalimbali inayotolewa kwa wanachama kujikwamua kimaisha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha

Afisa Masoko wa LPF James Mlowe akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kuwa tayari mfuko huo umeanzisha mkopo wa maisha popote na LAPF ambao unalenga kuwasaidia watumishi wa umma hususan wale walioajiriwa maeneo ya vijijini ili waweze kuanza maisha na kuwatumikia watanzania bila vikwazo vya kiuchum.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...