Mama Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
akiwa na mwanae Mhe. Makongoro Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari wakati walipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 27, 2016.
Mama Maria, ambaye hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana mwenye furaha kufika darajani hapo akisema kuwa ndoto ya miaka mingi iliyoanzishwa na hayati mumewe imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina la Mwalimu na siyo yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na vijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa hili la Tanzania.
Mama Maria, ambaye hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana mwenye furaha kufika darajani hapo akisema kuwa ndoto ya miaka mingi iliyoanzishwa na hayati mumewe imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina la Mwalimu na siyo yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na vijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa hili la Tanzania.
Mama Maria Nyerere na msaidizi wake pamoja na Mwanae Mh. Makongoro Nyerere wakitembelea Daraja hilo leo kwa furaha na fahari.
Mke wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Maria Nyerere
ametembelea Daraja la Nyerere linalounganisha eneo la Kigambaoni na Kurasini Jijini
Dar es salaam na kuipongeza serikali na wananchi wote wa Tanzania kwa kufanikisha
ujenzi wa Daraja hilo kubwa na la kisasa kwa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.
Mama Maria Nyerere aliyeongozana na Mwanae Mheshimiwa Makongoro Nyerere
amesema kukamilika kwa daraja hilo ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni
254.12 kumekamilisha mpango wa miaka mingi ulioanzishwa na Hayati Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa na nia ya kujenga daraja katika eneo hilo
la mkondo wa bahari lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti haikuwezekana.
Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuamua Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere
kwa heshimu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na
amebainisha kuwa uamuzi huo utaviwezesha vizazi vijavyo kutambua juhudi
zilizofanywa na mmewe katika ujenzi wa nchi.
"Mimi ninamshukuru sana Rais kwa maana ilikuwa lipewe jina lake, lakini yeye Mungu
akamjaalia akasema kwamba hapana tukumbuke tulikotoka, kwa hiyo najisikia vizuri
sana, na familia nayo inajisikia vizuri sana, lakini zaidi na watanzania wanajisikia vizuri
sana, kwa maana watakuwa wanaulizana Nyerere alikuwa ni nani?" Amesisitiza Mama
Maria Nyerere.
Daraja la Nyerere lenye urefu wa meta 680, upana wa meta 32, njia sita za magari na
barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 2.5, lilifunguliwa na Rais wa awamu ya tano
Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 19 Aprili, 2016 na linakuwa kiunganishi muhimu kati
ya Kigamboni na katikati ya Jiji la Dar es salaam.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Aprili, 2016
The mdudu, Asante sana MAMA na family yako kwa ujumla tupo pamoja katika harakati za kuijenga Tanzania yetu
ReplyDeleteNilitegemea kuona msongamano wa magari,!
ReplyDeleteWatanzania tuleni mihogo, ili nchi nzima ienee madaraja makubwa na flyovers. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MBARIKI RAIS JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.
ReplyDeleteNyerere Bridge: A beautiful piece of work, and we will keep it that way all day, all night.
ReplyDeleteNimefurahi kweli daraja hilo kupewa jina la Baba wa Taifa. Namshukuru Rais wetu kufanikisha hilo. Namshukuru Mama wa Taifa letu kupokea zawadi hiyo kwa ukunjufu. Ninafarijika pia kuona mifumo ya kiuchumi na kijamii mbali mbali ya Baba wa Taifa aliyoianzisha na kuilea inazaa matunda ya kujenga Taifa letu, mfano wa NSSF, NHC n.k.
ReplyDeleteHizo ndio sera za CCM. Magufuli hoyee, CCM hoyee!