TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imewafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya; aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Mori Sinare pamoja na Aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sioi Graham Solomon. 

Washtakiwa wote wanashtakiwa kwa makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha  Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na. 12 ya Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.

Mashtaka hayo yalisomwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mhe. Hakimu Emirius Mchauro. Kwa upande wa Jamhuri kesi hii inasimamiwa na Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Serikali Herman Tibabyekomia, Christopher Msigwa na  Mwendesha Mastaka wa TAKUKURU Stanley Luoga. Washtakiwa wanatetewa na Wakili wa Kujitegemea Ringo Tenga, Rosai Mbwambo, Semo na Nyaisa. 

Washitakiwa wote watatu wamepelekwa rumande, wamekosa dhamana kwani  Kifungu Na. 148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) Kinazuia utoaji wa dhamana kwa washtakiwa wa Utakatishaji wa fedha haramu. Kesi hii itatajwa tena tarehe 8/4/2016.

IMETOLEWA NA 
OFISI YA AFISA UHUSIANO 
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU 
1 APRIL, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. The mdudu, tupa lupango mifisadi mikubwa hiyo ndio maana miyaka nenda ludi uchumi wetu umedumaa kwa sababu ya hii mifisadi tupa lupango wote kisha malizao zote za kifisadi zitaifishwe hii safi sana Tanzania mpya hiyo yaja #shikaMooMagufuli

    ReplyDelete

  2. Shikamoo Rais wetu mpendwa Magufuli, hapa kazi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...