Na Ally Daud-maelezo

Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. John Kijazi ameutaka uongozi wa hospitali ya Mwananyamala kuhakikisha kuwa dawati la malalamiko kwa wagonjwa linafanya kazi masaa 24 ili kuboresha huduma katika hospitali hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kupokea msaada wa magodoro Dkt. Kijazi amesema kuwa wagonjwa wanatakiwa kuhudumiwa kwa wakati na kusikilizwa malalamiko yao muda wote wanapopatwa na changamoto hospitalini hapo ili kuweza kuboresha huduma kwa watanzania.

“Nimepata malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walipata matatizo usiku wa kuamkia leo na hakukuwa na mtu wa kuwasikiliza kwa wakati na kushindwa kupata huduma bora walipokuwa na shida hivyo naagiza uongozi kuhakikisha dawati la malalamiko kufanya kazi masaa 24 ili kuondoa kero za Wagonjwa wote”.alisema Dkt Kijazi.

Aidha Dkt. Kijazi ameushukuru uongozi wa Umoja wa Makanisa ya Pentekoste kwa kutoa msaada wa magodoro 50 yenye thamani ya shilingi milioni 1.631 ili kuendeleza huduma bora kwa wagonjwa wa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.

Akipokea msaada huo Dkt. Kijazi alisema kuwa anawaomba viongozi wa Umoja huo na taasisi zingineziendelee na moyo wa kuchangia kwenye shughuli za kijamii kadriwanavyoweza ili kuifikisha Tanzania salama katika kilele cha mafanikio.

“Nawaomba Umoja wenu, taasisi na wadhamini mbalimbali kuweza kusaidia kuinua na kukuza huduma bora za kijamii ikiwemo mahospitalini ili kusaidia serikali kupiga hatua katika kupambana na changamoto ya vifaa zinazoikabili hospitali ya Mwananyamala” aliongeza Dkt. Kijazi.

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi amesema kuwa ana Imani na Serikali ya awamu ya tano katika kutatua kero za wananchi hususani katika Wilaya yake kwani ameshaona mfano wa kupokea msaada huo na kuungwa mkono na Katibu Mkuu Dkt. John Kijazi kwa kushirikiana vizuri kwenye shughuli hiyo.

“Nafurahi kukutana na kushirikiana kwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi katika shughuli za kijamii hususani katika hili la kuendeleza huduma bora zitolewazo na hospitali ya Mwananyamala ili kuifikisha mbali Tanzania mpya” alisema Bw. Hapi.
Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi katikati akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani katika hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika katika hospitali ya Mwananyamala wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi na wa kwanza kushoto ni katibu Tawala wa Mkoa Bi. Theresia Mbando.
Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi katikati akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi na wa kwanza kulia na wa kwanza kushoto ni katibu Tawala wa Mkoa Bi. Theresia Mbando kuelekea wodini kusalimia wagonjwa wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika katika hospitali ya Mwananyamala .
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi wa kwanza kushoto akimsikiliza mmoja wa wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali ya Mwananyamala akitoa kero zake kuhusu hospitali hiyo wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika katika hospitalini hapo.
Baadhi ya magodoro yaliyopokelewa hospitalini hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...