Na Ally Daud- maelezo
Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama vinazidi kupungua kutoka siku hadi siku katika kufikia malengo ya milenia .
Akizungumza hayo katika hafla fupi ya kuzindua maonesho ya picha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kufikia malengo ya milenia kwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama.
“Tumefanikiwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama ili kufikia malengo ya milenia kwa upande wa afya kupitia mfumo wa kujiunga na bima ya afya kwa jamii” alisema Dkt. Mbando.
Mbali na hayo Dkt Mbando amesema kuwa amewakaribisha wananchi wote hususani wakazi wa Dar es salaam kuudhuria maonesho hayo yaliyofunguliwa leo yenye kauli mbiu ya “Huduma Bora kwa Afya Bora”yatayofikia kilele mpaka Juni 10 mwaka huu ili kupata ujumbe zaidi kupitia picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini.
Aidha ameipongeza Serikali ya Ujerumani kupitia ubalozi wake kwa kushirikiana vizuri na Serikali ya Tanzania na kukubaliana kupata msaada wa Euro milioni 47 kwa muda wa miaka mitatu ijayo katika kuinua sekta ya Afya.
Kwa upande wa balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke amesema kuwa mchango wa Serikali ya ujerumani kwa sekta ya afya Tanzania utaendelea kuwa sehemu ya mpango wa ushirikiano wa nchi mbili ili kuinua sekta hiyo nchini.
Balozi
wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke kulia akikata utepe kuashilia kuanza
rasmi kwa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni
10 mwaka huu jijini Dar es salaam na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto ,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando.
Balozi
wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke akiongea na waandishi wa habari na
Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) hawapo
pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho
ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto ,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando akiongea na waandishi wa habari
na Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH)
hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika
Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mshauri
wa ufundi kutoka Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH)
Dkt. Baltazar Ngoli wa kwanza kulia akitoa maelekezo ya picha kwa Balozi
wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke wa pili kulia pamoja na Mwakilishi wa
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto ,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando wa tatu kulia wakati wa ufunguzi
wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es
salaam.
Wadau
mbalimbali wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH)
wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya
Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt.
Margaret Mbando hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha
yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es
salaam.Picha zote na Ally Daud-Maelezo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...