Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
BAADA ya kuiongoza timu yake kutetea ubingwa wa ligi kuu, fainali ya kombe la FA na kuingia hatua ya makundi nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub 'canavaro' (Pichani)amesema kuwa watahakikisha wanapiga kufa na kupona kuweza kuisaidia timu yao kuingia hatua ya nusu fainali kwani kama watafanya vizuri michezo mitatu ya mwanzo basi watakuwa wameweza kuvuka makundi.

Canavaro amesema mwaka huu wamekuwa na kikosi bora ambacho kimekuwa kinaleta ushindani wa hali ya juu katika kila mechi watakayokuwa wanacheza na hicho kinakuwa ndiyo msingi mkubwa kwao wa kufanya vizuri zaidi.

"Tumeingia hatua ya makundi na tunajua ni moja ya hatua ngumu sana tuliopo ila michezo mitatu ya mwanzo tukipata alama basi tutaingia nusu fainali na hatimaye fainali kabisa na ikiwezekana tutaleta kombe nchini,"amesema Canavaro. 

Na katika kujiandaa zaidi kocha mkuu Hans Van De Pluijm anajua ni wapi atapeleka kikosi kwa ajili ya maandalizi zaidi kwani Juni 17 tunaanza kucheza na Mo bejala nchini Algeria na siku 10 baadae kutakuwa na mechi nyingine dhidi ya TP Mazembe Jijini Dar es salaam.

Amesema, kwa sasa wachezaji wote wanatakiwa kujiweka sawa na kuwazia mashindano yaliyokuwa mbele yao katika kipindi hiki kwani kufanya vizuri kwao kutalitambulisha taifa zaidi.

Wakati huohuo,
Timu ya Taifa imeondoka Alfajiri ya leo huku nahodha huyo wa zamani Canavaro akiwa hajajumuika na kikosi hicho kinachonolewa na Charles Boniface Mkwasa na kuendelea kuweka msimamo wake wa kutokuchezea timu ya taifa kwani ameshaamua na tayari barua ipo TFF.

"Nimeshaweka msimamo wangu kuwa sitachezea tena timu yaTaifa na ndio maana sijajiunga nao kuelekea Kenya kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Harambee Stars,"amesema Canavaro.

Toka kujiengua kwa Canavaro,Mkwasa anamuita kwa mara ya kwanza baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mechi alizocheza akitoka katika majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani miezi mitatu bila kucheza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...