Ipo kauli isemayo "Mfupa Uliomshinda Fisi" ikiashiria jambo gumu mithiri ya mfupa mgumu ambao umemshinda fisi ambae ni mnyaba bingwa wa kutafuna mifupa ya kila aina.

Ndivyo unaweza kusema ukiitazama picha hizi, kwani suala la kuzagaa ovyo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Machinga jijini Mwanza, ni mfano halisi wa mfupa ulioshindikana kutafunwa na halmashauri ya jiji la Mwanza.

Mara kadhaa juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuwaweka wafanyabiashara hao katika mpangilio mzuri kwa ajili ya wao kufanya biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kwani mafanikio yake yakishindwa kuwa ya kudumu licha ya nguvu kubwa kutumika.

Kabla ya kipindi cha kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana, halmashauri ya jiji la Mwanza ilifanikiwa kuwaondoa machinga katika maeneo yasiyo rasmi lakini baada ya kampeni kuanza, machinga walirejea mitaani kwa kasi ya ajabu na hakuna aliewagusa tena ambapo hivi sasa kila kona ya jiji la mwanza machinga wamezagaa ovyo.

Baadhi ya Machinga jijini Mwanza wanaomba sekta hiyo kuboreshwa ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo kukosa maeneo maalumu kwa ajili ya wao kufanyia biashara hatua ambayo itasaidia kuondokana na kadhia mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mgambo wa jiji wanaokuwa wakiwaondoa katika maeneo yasiyo rasmi kufanyia biashara.

Bonyeza HAPA Kwa Picha Zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...