Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
MSHAMBULIAJI wa Simba SC Mussa Hassan Mgosi amesema, kuelekea katika usajili  wa wachezaji wapya viongozi  wanaqtakiwa kuangalia ambao wanahaki ya kuitetea simba na sio kusajili mchezaji kwa sababu ya jina lake.

Mgosi amesema, Klabu inatakiwa kusajili wachezaji ambao wataipa Simba kile kitu ambacho kinakihitajika ili kuiweka timu katika nafasi nzuri.

Mgosi amesema, wachezaji wa kigeni wanahitajika lakini waangaliwe kama ni watu aina gani wanahitajika na wanauwezo wa kuitetea timu kwa kazi watakayoifanya.

"Mchezaji wa kigeni anatakiwa kufanya kazi ya ziada ambayo itamzidi yule mchezaji mzawa ili kuweza kuweka utofauti kati ya mchezaji wa kimataifa na mzawa katika klabu,"amesema Mgosi. Hilo limekuja baada ya wachezaji wa kigeni wa timu hiyo kucheza chini ya kiwango ukilinganisha na wazawa na wengine kuishia kuishia kukaa benchi.

Mgosi amesema, viongozi wanatakiwa kuangalia makosa yaliyotokea katika msimu uliopita na kupelekea timu kushindwa kufikia malengo ili kuyarekebisha na hata usajili utakapofanyika uwe wa kueleweka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...