Kuongezeka kwa migogoro ya matumizi ya Ardhi nchini kumesababisha umuhimu wa kupata Sera ya Taifa ya Ardhi ambapo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inawapa fulsa wadau wote kushiriki katika kutoa maoni yao ili kupata Sera ya Ardhi iliyoridhiwa na watu wengi nchini. 

Katika kufanikisha kazi hii Wizara ya Ardhi inakutana na wadau hawa walioko nchi nzima ambao wanawakilishwa na kanda nane za ardhi nchini.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wakishiriki kujaza dodoso la maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995.
Bwana James Mwamfupe wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) akitoa maoni yake katika kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 wakati wa mkutano wa wadau uliofanyika mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wadau wa Ardhi wa mkoani Dodoma wakishiriki kupitia na kuiboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 ili kukabili changamoto zinazoikabili sekta ya Ardhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...