Baadhi ya Wafanyakazi wa  MultiChoice-Tanzania wakiwa katika vazi la kiafrika siku ya kuazimisha Africa day.

Jinsi Chaneli za TV za Barani Afrika zilivyofanikiwa kuelezea habari za Afrika katika mtazamo wa Kiafrika. 

Haukasiriki unapoangalia onyesho katika televisheni au filamu ya kutoka Afrika au kumhusu muafrika na kisha ukatahamaki, “ Hii haina chochote kinachofanana na Afrika ninayoijua?”. Kwa miongo kadhaa, tasnia ya burudani ya filamu na televisheni imetawaliwa na simulizi zenye maudhui ya nchi za Magharibi- hata pale zinapokuwa za kutoka Afrika na kwa ajili ya Waafrika. Kwa bahati nzuri, ndani ya miaka kadhaa iliyopita, tumeona mabadiliko japo ya taratibu lakini ya uhakika, ya simulizi zenye uhalisia kuhusu Waafrika zikisimuliwa kuhusu bara letu.

MultiChoice tunajisikia fahari kutokana na ushiriki wetu katika mabadiliko na maendeleo haya tangu kuanzishwa kwetu barani Afrika miaka 20 iliyopita. Mojawapo ya malengo yetu ya msingi ni pamoja na kuhakikisha kwamba huduma zetu zinawaendeleza wateja wetu kwa kuwaletea maudhui ambayo wanaweza kuyahusisha nayo na maisha yao ya kila siku. 

Lengo hili linatukumbusha dhamira yetu ya kuendelea kuunga mkono na kuendelea kuwekeza katika tasnia ya burudani barani Afrika na kuonyesha vipaji vya waafrika kupitia chaneli za hapa barani Afrika za MNet. Kutoka Nollywood mpaka Riverwood, tunaamini katika kusimulia na kuelezea habari au simulizi za Ki-Afrika ambazo watazamaji wetu wanaweza kuzihusisha nazo na maisha yao ya kila siku. Siku ya Afrika inapokaribia tarehe 25 May mwezi huu, tunasheherekea wasimulizi mbalimbali kutoka Afrika ambao wanachangia katika ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni ya Afrika.

Watazamaji wetu wametuamini kuwa waangalizi na wahifadhi wa simulizi za kiafrika na kuhakikisha panakuwa na simulizi zenye uwiano kuhusu Afrika. Kimsingi hakuna simulizi moja ambayo inafafanua au kuelezea kila kitu kuhusu bara letu na ndio maana chaneli zetu za zinazolenga bara la Afrika ambazo zinajumuisha Africa Magic, Maisha Magic Bongo, Maisha Magic East (E36) na Zambezi Magic, Mzansi Music na Mzansi Bioskop- zimeahidi na kujizatiti katika kuelezea simulizi za Afrika kama zilivyo. Chaneli hizi zinaleta mtazamo tofauti kuhusu maisha ya Afrika ambayo watazamaji wake wanaweza kuyahusisha na maisha yao ya kila siku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...