Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
KOCHA Mkuu wa timu ya Ruvu Shooting, Tom Olaba ameweka msimamo wake wa kutaka nyota saba wapya atakaowajumuisha ndani ya kikosi chake msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara huku malengo yake yakiwa ni golikipa, beki wa kati na pembeni, kiungo mshambuliaji na mkabaji na mshambuliaji. 

Maafande hao wamekuwa wa kwanza kupanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Lipuli na kufikisha pointi 31 ambazo zilikuwa ngumu kufikiwa na timu yoyote kwenye Kundi B. 

Msemaji wa timu hiyo Masau Bwire amesema kocha  ametoa mapendekezo hayo ili kuhakikisha kikosi chake kinakuwa bora msimu ujao na kama viongozi wa timu hiyo watahakikisha mapendekezo ya mwalimu yanafanyiwa kazi ili wapate kikosi bora. 

"Mwalimu ameomba kuongezewa wachezaji saba atakaowajumuisha katika kikosi chake msimu ujao ili kuongeza nguvu, na uongozi utafanikisha hilo kwa asilimia 100", amesema Masau. Nanaamini mapendekezo hayo ya Olaba yataleta mafanikio makubwa kwa timu yao na kudhihirisha kuwa walishuka daraja kwa bahati mbaya. 

Akizungumzia mazoezi ya timu yao, Masau amesema kuwa vijana wote wameshawasili kambini na wanaendelea kujifua katika uwanja wao wa Mabatini uliopo Kibaha, Pwani. "Mazoezi yanaendelea vizuri kwa ailimia 90 kwani vijana wanaonesha moyo wa kujituma wakiwa na dhamira moja tu ya kuhakikisha wanafanya vizuri msimu ujao wa ligi kuu", amesema Masau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...