Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Halfan Mshiro pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema wakiokota baadhi ya uchafu katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta walipozuru kaburi hilo katika kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni mtoto wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi na kulia ni Naibu Meya Bw. Salum Faisal.
Mtoto wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi (watatu kulia) akiongoza dua ya kumuombea baba yake hayati sheikh Kaluta Amri Abeid wakati ujembe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema (kushoto mbele) akizungumza wakati ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Nuru Halfan Mshiro.
Ni maoni yangu tu asikwazike yeyote. Nadhani inapendeza zaidi na ndivyo itakiwavyo kiimani, khususan kwa wanawake kujistiri vile itakiwaivyo inapotokea ziara ya kwenda kuzuru makaburi na khasa yale yakhusuyo Imani hiyo. Ni wajibu kukumbushana mara tunapoghafilika. In Sha Allah.
ReplyDeleteHaya tena hakuna jema!
ReplyDeleteMdau wa pili hata hilo liilloelezwawa hapo juu ni jema kwa wenye imani yao. Yawezekana ikawa baya kwako, l jema kwa wenzako.
ReplyDelete