MAMALAKA ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi(VETA) ikishirikiana na wadau kutoka viwanda vya umeme na umeme wa magari wametoa maendeleo ya mradi huo kwa wadau wa viwanda.
 
Hayo yamesemwa Mkurugenzi wa kanda ya Dar es Saalam, Habibu Bukko wakati akizungumza na wadau wa viwanda vya umeme na umeme wa magari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa mafunzo hayo yanaumhimu mkuwa kwa viwanda kwani mafunzo hutolewa kwa umahili mkubwa kwa walichaguliwa kujifunza mafunzo hayo kutokana na mahitaji ya kiwanda.
 
Bukko amesema kuwa mafunzo yanayotolewa ni ya vitendo zaidi (Hands & Skills) chini ya Mradi wa ushirikiano baina ya VETA na Kampuni ya Handwerkammer Humbarg ya Ujeruman.
 
Amesema kuwa utaratibu wa mafunzo hayo yamaendaliwa kutoka na vyuo vya mafunzo ya ufundi Stadi.
Mkurugenzi wa kanda ya Dar es Saalam, Habibu Bukko akizungumza katika mkusanyiko wa wafanyakazi,viongozi wa Veta pamoja na (Wanagenzi) wanafunzi wanafanya mafunzo yao katika viwanda mbalimbali hapa nchini waliojiunga katika mradi wa wanagnizi(APPREUTICESHIP) jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa mradi huo unawajulisha wanafunzi wanataka kujiunga na mafunzo hayo katika chuo cha Veta na kufanya kazi katika viwanda mbalimbali hapa nchini kuwa mafunzo hayo hayana gharama yoyote na unajifunza katika kiwanda unachohitaji kutokana na taaluma yako.
 

Meneja wa Mradi wa Appreaticeship kutoka kampuni ya Handwerkammer Humbarg ya Ujeruman, Maltin Mac Mahon akizungumza na wadau wa Veta jijini Dar es Salaam leo na akielezea jinsi alivyowafundisha wanafunzi wa veta ambao wapo na ambao hawapo viwandani hapa nchini kutengeneza vitu vya umeme pamoja na umeme wa magari hapa nchini pamoja na vitu mbalimbali vilivyopo katika viwanda mbalimbali kutokana na mahitaji ya kiwanda husika.
Wanafunzi wanafanya mafunzo katika viwanda mbalimbali hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo cha mafunzo ya ufundi (VETA) jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...