Na Woinde Shizza, Karatu.

Watu wa Jamii ya Wawindaji waokota matunda na walina asali kutoka kabila la Wahadzabe katika kijiji cha Endamagh wilaya ya Karatu, wamelalamika kitendo cha kutengwa kuingizwa kwenye mpango wa ruzuku kwa kaya masikini, unaoendeshwa na TASAF wakati wao ni jamii masikini zaidi, kwani kati yao ni kaya saba tu ndizo zilizo ingizwa kwenye mpango huo, hivyo wanalazimika kugawana kiasi kidogo wanacho  kipata.

Watu hao wa kabila la Wahadzabe wametoa kauli hiyo  katika kijiji cha Endamash, walipotembelewa na maafisa wa TASAF kutoka Makao Makuu, pamoja na wawakilishi wa Benki ya Dunia, ambapo wamedai sasa wanalazimika kugawana fedha zinazo tolewa kwa kaya saba kwakuwa wote hawana uwezo na matunda na wanyamapori wameadimika kutokana na ukame.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Billar Bird amesema amesikitishwa na hali waliyo nayo watu hao, lakini amechukua maombi yao na atayafikisha kwenye kikao cha nchi wafadhili wanaotarajia kukutana mwezi ujao.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema kasoro hizo zimetokana na tabia ya jamii hiyo ya kuhamahama ndiyo maana walikosa fursa hiyo lakini  TASAF itaangalia namna ya kuwasaidia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...