Mkuu wa Mkoa  Dar es salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule Feza wa nchi 15 waliokuja kwaajili ya kutangaza utamaduni wa nchi zao jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
WATANZANIA wametakiwa kuwa wazalendo katika kutangaza utamaduni katika nchi mbalimbali  kwa kutumia  lugha ya Kiswahili na kuacha kutumia tamaduni za nje ambazo zinachangia mmomonyoko wa maadili.
 
Hayo ameyasema leo Mkuu wa Mkoa  Dar es salaam, Paul Makonda alipotembelewa ofisini kwake na wanafunzi wanaosoma Shule za Feza kutoka nchi 15 waliokuja nchini kutangaza utamaduni wao hivyo hata Tanzania tunaweza kutanga lugha yetu ya Kiswahili..
 
Amesema watanzania wengi wamekuwa wakiiga tamaduni za kigeni na  kusahau utamaduni wao ambao ungeweza kuwatambulisha katika nchi nyingi na kuijenga sifa ya nchi  kwa utamaduni wa lugha yatu adimu ya Kiswahili.
 
Makonda amesema kuwa ni jambo la kushangaza kuona watu kutoka nchi mbalimbali wakija Tanzania kutangaza utamaduni wao na watanzania wakikaa na kuishia kuiga tamaduni za watu na kuacha tamaduni zao kupotea huku nchi zingine zikiwa mbele katika kutangaza utamaduni huo..
 
Amesema kuwa utamaduni mkubwa ambao tunaweza kuutangaza ni lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo pekee inaweza kuitangaza nchi yetu duniani kote na ikajenga heshima ya nchi kuliko kufuata tanmaduni ambazo haziwajengi watanzaniazaidi ya kuwaharibu” alisema Makonda.
 
Nae Mkuu wa shule ya Feza Tanzania Kadik Dakicek, ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo wakishirikiana na International Festival Language and Culture alisema, madhumuni makubwa ya ujio huo wa wanafunzi hao ni kutangaza tamaduni zao na Tanzania ndio mwenyeji wa shuguli hiyo kwa mwaka huu.
 
Tamasha kama hili la kutangaza utamaduni katika nchi mbalimbali na mwaka huu tunafuraha kuona Tanzania inakuwa mwenyeji wa tamasha hili tunaamini kupitia tamasha hili nchi itajifunza mambo mbambali ambayo yatawasaidia kutangaza utamaduni wetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...