Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hivi hawa madereva wetu khususan kwa haya mabasi ya mwendo kasi, ndio kusema hawakupatiwa mafunzo ya kutosha?, hawana uzoefu mzuri na mabasi ya aina hiyo?, au wanadhani kwa vile yametengewa' special lane' ndio hakuna kuchukuwa tahadhari yeyote ni ku flow tuuu! au imekaakaaje? Ukiangalia ndio kwanza yameanza kazi barabarani, lakini imekuwa kitahanani kitupu, ajali n.k. Hawakukosea wahenga wetu pale waliponena...mzowea Punda Farasi hamuwezi; mana mpaka akija kumzowea atapita akipinduka nae huku na kule akitaamaki makovu mwili mzima.

    Japo ajali haina kinga, lakini tuwe makini madereva tuwapo barabarani, haijalishi una right ya kutumia njia au laa!, we have to be aware kwa situation yeyote ile ambayo ina indicate hazard ili kuepuka na kupunguza ajali barabarani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 29, 2016

      Sawa baba shangaa mwendo kasi, ngojea reli zitengemae udhanie ukijiingiza relini dereva treni atachukua tahadhari kwa niaba yako!

      Delete
  2. AnonymousMay 29, 2016

    Huyo alienda kutafuta nini kwenye njia ya mabasi.....watu hawasikii kilicho baki ni wagongwe tu labda watapata fundisho. Na wakisha gongwa walipe garama zote pia....

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2016

    DUUUUUU HI KALI MDAU NAMBA TATU NIMEKUPATIA MARKS 100 KWA 100,UMENIVUNJA MBAVU FUNDISHA KABISA WATU HAWAELEWI HUYO NAMBA MOJA YEYE ANALETA TU UTUMBO HAPA

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2016

    kuna tofauti kati ya treni na haya mabus. Dereva wa hili basi ana uwezo wa kuchukua tahadhari zote kujiridhisha kuwa ni muafaka kupita. Hata sisi wenye magari sio kwa sababau taa zimeruhusu unatiririka tuuu tungekuwa tumeshaisha. Madereva wa haya mabus watambue kuwa kipindi hiki cha mpito ni lzm kuwa makini sana. Elimu itolewe kwao na itolewe kwa wananchi wote.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2016

    Wewe mtoa maoni wa kwanza inawezekana ni wale wale wasiosikia,swali hiyo njia ni maalumu kwa hayo mabasi sasa hilo gari dogo limeingia kufanya nini?na hayo mabasi breki zake siyo kama unazofikiri za ghafla,acheni hizo njia za mabasi la sivyo mtaendelea kugongwa tu

    ReplyDelete
  6. Yaaani watu wengine ni pumba kabisa barabara za magari ya mwendokasi halafu unasema wawe makini, inakuaje hao wengine watumie barabara ambazo zimetengwa kwa magari maalumu, wagongwe tu ili wajifunze kwa njia ngumu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 03, 2016

    Mdau wa sita hapo juu ungeyasoma kwa kina na kuyaelewa maelezo ya mdau wa kwanza ndio mana akasema isiwe sababu kwa kuwa yana barabara yake maalum ya mwendo huo ndio iwe chambo cha kutozingatia usalama yawapo safarini. Hapo hakuna cha kusikia swali wala kutowa majibu ni jinsi uelewa wako wewe ulivyo finyu ndio mana hukuipata pointi yake na moja kwa moja ukakimbilia kuivamia hoja. Nchi za wenzetu wana mpaka ma 'double decker' na bara bara zao maalumu kama hizo lakini inapotokea dharura yanasimama na kufunga brake kama magari mengine seuze hayo, usidhani kila mtu ndio kwanza kuyaona hapo bongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...