Tanzania
Network Information Centre (tzNIC) au Rajisi ya dot tz ni kampuni inayoendesha
na kusimamia rasilimali ya nchi (dot tz) kwa ajili mawasiliano kupitia mtandao
wa Intaneti. tzNIC inapenda kuuarifu umma wa watanzania kuwa imetenga siku za Jumatatu
(27 Juni 2016) na Jumanne (28 Juni 2016) kutoa elimu kwa
umma juu ya kazi zake, manufaa ya matumizi ya majina ya kikoa cha dot tz (.tz
domain names) na namna bora ya kuhama kutoka matumizi ya majina mengine ya
vikoa kama dot com na dot org kwenda kikoa cha dot tz. Katika kipindi hicho
tzNIC pia itapokea maoni mbalimbali juu ya uboreshaji wa huduma zake na nini kifanyike ili
watanzania wengi wasajili na kutumia majina ya kikoa cha dot tz kwa ajili ya
biashara zao, huduma zao na matumizi binafsi.
Tukio
hili litafanyika katika ukumbi wa mikutano wa tzNIC, Ghorofa ya 8, LAPF
Millennium Towers, Kijitonyama, Dar es Salaam kuanzia saa 3 mpaka saa 10 jioni.
Kabla ya tukio hili tzNIC itatoa maelezo ya utangulizi kupitia kipindi cha
Jambo Tanzania (TBC) siku ya Ijumaa (24 Juni 2016) au Jumatatu (27 Juni 2016)
asubuhi.
Kwa
wale wa mikoani na watakaoshindwa kufika wanaweza kutupigia simu (022 2772659
au 022 2772660) au kutuandikia barua pepe kupitia manager@tznic.or.tz) au info@tznic.or.tz
WOTE MNAKARIBISHWA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...