Na Ally Daud-Maelezo
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) imeadhimia kuimarisha  usafiri wa anga ili luleta huduma bora na kuwapa amani  wananchi wanaotumia usafari wa anga katika Jumuiya hiyo.
Hayo yamesemwa  leo na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mheshimiwa  Makame Mbarawa alipokuwa  akifungua  Mkutano wa 19  wa Kamati ya SADC ya usafiri wa Anga uliofanyika jijini Dar es salaam. 
“Mkutano huu unalenga kuadhimia kuimarisha usalama wa anga katika nchi za Jumuiya ya SADC, kwa kuwa unahitajika sana kwa wananchi  ili kuongeza shughuli za kiuchumi na kijamii na kuleta maendeleo ya nchi wanachama” alisema Mbarawa
Ameongeza kuwa “ni lazima tuadhimie mambo yatayoleta maendeleo na huduma bora katika usafiri wa anga kwa jumuiya ya SADC ili kujenga uhusiano na malengo yaliyo bora kwa maendeleo ya nchi zetu.”  
Kwa upande wake,  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Bwana Hamza Johari amesema kuwa mkutano huo unalenga kuhakikisha wanafikia na kutekeleza malengo  Jumuiya ya usafiri wa anga wa kimataifa (ICAO) katika kuboresha huduma  za usafiri huo.
“Ni lazima tuyafanyiekazi   maadhimio ya  mkutano huu  ili kuboresha huduma kwa kiwango cha kimataifa pamoja na kuleta unafuu kwa watumiaji wa usafiri wa anga” alisisitiza  Bw. Johari.
Naye,  Mwenyekiti wa SADC Bw. Geoffrey Moshabesha amesema  kuwa  kamati hiyo inajipanga kuunda taasisi ya kiusalama ili kusimamia mifumo yote kwa nchi nzima ili kuweka mazingira mazuri kwa watumiaji wa usafiri wa anga.
Jumuiya ya SADC imeweka  mikakati ya kutekeleza maadhimio hayo katika kuleta usalama wa anga pamoja na kutunza mazingira ili kuboresha huduma kwa watumiaji wa usafiri wa anga kwa nchi wanachama.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Makame Mbarawa akiongea na wadau mbali mbali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) hawap[o pichani katika ufunguzi wa mkutano wa 19  wa kamati ya SADC usafiri wa anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
 Wadau mbali mbali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Makame Mbarawa hayupo pichani katika ufunguzi wa mkutano wa 19  wa kamati ya SADC usafiri wa anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Makame Mbarawa  akiwa katika picha ya pamoja na Wadau mbali mbali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) baada ya ufunguzi wa mkutano wa 19  wa kamati ya SADC usafiri wa anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
Picha zote na Ally Daud- Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...