Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH), Profesa  Lawrence Museru leo amekutana na Madaktari  wa MNH  ikiwa ni mkakati wa kukutana na watumishi kwa lengo la kuwasikiliza na kujibu kero zao.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa CPL uliopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru amewapongeza  madaktari hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kuimarisha utoaji huduma kwa wagonjwa na kwamba hali hiyo imechangia MNH kuongeza mapato yake.
Amesema kuongezeka kwa mapato ya Hospitali na kufikia Shingili Bilioni 4. 5 kwa mwezi kumetokana na kila mmoja kutimiza wajibu wake.
Amesema kutokana na mafanikio hayo,  MNH imewaongezea madaktari  wake posho mbalimbali  ili kuongeza tija katika utendaji, lakini pia hospitali  imeamua  kutenga Shilingi Milioni 800 kwa mwaka ili kuwapa mkono wa heri wastaafu wake  jambo ambalo awali halikuwapo.
Hata hivyo amesema mbali na hatua hiyo, pia MNH imefanikiwa kulipa malimbikizo mbalimbali ya stahiki  za wafanyakazi wake ikiwamo  pesa za likizo kwa madaktari pamoja na watumishi wengine kwa ujumla.
“ Awali changamoto kubwa ilikuwa ni ucheleweshaji wa stahiki za wafanyakazi kwa Madaktari na watumishi wengine, lakini katika hilo tumefanikiwa kwani tunaenda nalo vizuri na tumelipa malimbikizo hayo “ amesema Profesa Museru.
Akielezea mipango ya MNH  Profesa Museru amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina mipango mbalimbali ya kuendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vitanda vya Chumba ya wagonjwa Mahututi-ICU-, kuongeza ICU ya watoto pamoja na kina Mama wajawazito.
Kaimu Mkurugenzi huyo Mtendaji wa MNH kesho Juni 23, 2016 atakutana na Wauguzi pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru LEO amekutana na madaktari bingwa wa hospitali hiyo kwa ajili ya kuwasikiliza na kujibu kero mbalimbali.
 Baadhi ya madaktari bingwa wakimsikiliza Profesa Museru baada ya kukutana nao LEO kwenye ukumbi wa CPL katika hospitali hiyo. 
 Madaktari Bingwa wakimsikiliza Profesa Museru LEO kwenye ukumbi wa CPL.
 Dk Saidia Primos wa hospitali hiyo akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Dk Moa akiuliza swali baada ya kupewa nafasi kwenye mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...