Kikosi cha DarCity Veterans, kinachoongozwa na Mwanasoka wa zamani, Tippo Athuman Shaaban "Zizzou" (Wa nne kulia waliosimama) kikiwa katika picha ya pamoja, kabla ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Timu ya Boko Beach Veretans (BBV), uliopigwa Julai 24, 2016 kwenye Uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam. Mchezo huo uliowakutanisha pamoja wakombwe mbali mbali wa Soka nchini enzi hizo na sasa, ulikuwa ni wa burudani ya aina yake kutokana na uwezo mkubwa wenye ufundi wa hali ya juu ulioonyeshwa na wakongwe hao, ikiwa ni sehemu ya kuwahamasisha vijana wanaochipukia na hasa wale wenye vipaji vya Mchezo wa Soka kuupenda mchezo huo na kuucheza kwa utaalam wa hali ya juu, kwani mchezo huo ni Ajira na ni burudani pia. Mchezo huo ulimalizika kwa Timu ya DarCity Veterans kuwachapa Boko Beach Veretans (BBV) Bao 3-0, Mabao mawili yakiwekwa kimiani na Mshambuliaji Machachari wa DarCity, Juma Kaseja na huku moja likitupiwa na Kiugo mchezeshaji, Salvatory Edward baada ya kupata krosi nzuri kutoka kwa Akida Makunda. Pichani toka kulia waliosimama ni Kassa Mussa, Madaraka Seleman Kibode "Mzee wa Kiminyio", Salvatory Edward, Tippo Athuman, Ally Mpemba, Maalim Chomba, Idd Seleman Kibode na Meneja wa Timu ya DarCity, Ernest Nyambo. Waliochuchumaa toka kulia ni, Akida Makunda, Macocha Moshi Tembele, Shila Mjema, Shaban Kado, Juma Kaseja, Richardson Sakala, Ally Kakima pamoja na Zubeiry Katwila.
 Kikosi cha Boko Beach Veretans (BBV) chini ya Nahodha wake Mabe (kulia waliosimama).
 Mshambuliaji machachari wa DarCity Veterans, Shaban Kado akichuana vikali na mabeki wa timu ya Boko Beach Veretans (BBV), wakati wa Mchezo wa kirafiki, uliopigwa Julai 24, 2016 kwenye Uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam .
 Akida Makunda wa DarCity Veterans, akiwa katika ubora wake, mbele ya wapinzaji wake.
 Kiungo Mnyambuliko wa DarCity Veterans, Tippo Athuman Shaaban "Zizzou" akionyesha utaalam wake, katika mtanange huo wa kuvutia uliopigwa Julai 24, 2016 kwenye Uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...