Kama kawaida yake Globu ya Jamii imefanya jitihada za ziada ili kuachana na tetesi na maneno ya mitaani na kuwasiliana na maripota wake jijini Kinshasa ili kupata undani wa yanayomsibu mwanamuziki nguli wa DRC Koffi Olomide 'Mopao' kufuatia kisanga cha kutiwa mbaroni kwa kosa la kumshambulia mnenguaji wa bendi yake ya Quarter Latin aitwaye Pamela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya. 
Ripota wetu amegundua  kwamba sio kweli Koffi Olomide tayari ameshahukumiwa kwenda jela miaka 18,  ama kama wengine wanavyosema miezi mitatu na wengine mwaka mmoja. Ukweli ni kwamba amepelekwa jela kwa siku tano kabla ya kufika tena mahakamani kujibu shtaka la kujeruhi kwa kukusudia (intentional injury) na kufanya fujo hadharani. 
Baada ya kukamatwa leo Jumanne asubuhi nyumbani kwake Kinshasa alipelekwa mahakamani ambako amri ya kumweka jela kwa siku tano ikatolewa. 
Shtaka kuu analokabiliwa nalo Mopao ni kumuumiza dansa wake wa kike na  kufanya fujo hadharani. 
Video zifuatazo zinaonesha Mopao alipokuwa akitolewa mahakamani na kupelekwa gereza kuu la Makala. Video ya chini ni wakili wake akieleza mambo yalivyo. Wanaojua Kifaransa kazi kwenu...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2016

    Kesha pigwa mvua na nusu.....

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2016

    Shida kubwa za hawa jamaa ni kwamba wakisha kuwa matajiri na maarufu wanajisahau. Wafikiria kuwa wao ni majogoo na waweza kutenda chochote vile. Sasa akisota jela atakumbuka atokea wapi, majuto ni mjukuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...