Na Bashir Yakub.

Haki hizi zinatoka katika Sura ya 20, Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai kifungu cha 48 hadi 59. Ni haki ulizonazo ikiwa utazuiliwa na kuhojiwa  na polisi.

1. Ni lazima polisi akutajie jina lake pamoja na cheo chake kabla hajakuhoji. 

2. Lazima uambiwe tena kwa lugha inayoeleweka kosa ambalo unatuhumiwa nalo. Unaweza kuambiwa kwa maandishi au kwa mdomo.

3. Una haki ya kutaka kuitiwa mwanasheria , ndugu, au rafiki ambaye unaamini atakusaidia katika kutoa maelezo au kufanya mahojiano.

4. Ni kosa kulazimishwa kukiri kosa au kuandika kile askari anachotaka.

5. Baada ya kutaja jina lako na anuani yako una haki ya kutojibu swali jingine ikiwa utaona inafaa kufanya hivyo.

6. Una haki ya kukataa kujibu maswali yasiyo na staha au yanayolenga kudhalilisha au kuondoa utu wako au wa familia yako.

7. Hairuhusiwi kupigwa, kudhalilishwa, kuteswa unapohojiwa au unapokuwa kizuizini.

8. Una haki ya kupatiwa au kuwezeshwa kupatiwa matibabu ikiwa u mgonjwa au una jeraha wakati wa mahojiano au kizuizini.

9. Ikiwa aliyewekwa kizuizini ana umri chini ya miaka 16 basi mara tu baada  ya kukamatwa kwake afisa polisi aliyemkamata au mwingine ana wajibu wa  kuhakikisha anawasiliana na mzazi au mlezi na kumweleza kukamatwa , kituo alipo, na kosa alilokamatiwa.

10. Askari anayekuhoji ana wajibu wa kuweka katika rekodi/maandishi mahojiano yenu ili kusiwe na kuongezwa au kupunguzwa kwa yale uliyosema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...