Na Geofrey Chambua
1. Mzaliwa wa Februari 21. 1924; Komredi Robert Gabriel Mugabe Ni mtoto pekee aliyesalia katika familia yao kwani kaka zake wawili walifariki akingali mdogo sana na baba yake alitelekeza familia yao mnamo mwaka 1934 na kumlazimu mama yake kuolewa na mwanaume mwingine. Ingawa unamjua Mugabe kama Rais wa Zimbabwe ukweli ni kwamba Baba yake mzazi Gabriel Matibili ni Mmalawi aliyekua fundi seremala ila mama yake ambaye ndiye aliyemlea ni Mshona wa Zimbabwe kwa asili. 

2. Kwa miaka 92 amekua​ akitumia zaidi vyakula vya asili ya mimea (Vegetarian) chakula chake kikuu ikiwa ni maboga ingawa aghalabu hula nyama pori na hasa nyama ya ​S​imba na ​T​embo. Mugabe pia hatumii kileo wala kuvuta sigara

3. Huamka saa kumi alfajiri kila siku kwa mazoezi mepesi na hupenda sana kusikiliza BBC baada ya hapo, huenda hii ikaelezea kwa nini husinzia sana hata kwenye hadhara
4. Ana jumla ya shahada SABA. Digrii yake ya kwanza ni kutoka katika ​C​huo ​K​ikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika Kusini. Alisomea digrii zake zingine sita kwa njia ya masafa (Distance Learning) kati ya hizo mbili ​za Sheria ​akiwa gerezani. Kazi yake ya kwanza kabla ya kujiunga na siasa ni UALIMU na alianza kufundisha Chuo cha Ualimu Chalimbana nchini Northen Rhodesia (Zambia kwa sasa) kisha Apowa Sekondary nchini Ghana. Mugabe amekua akisisitiza sana katika elimu nchini mwake na ameiwezesha Zimbabwe kuweka rekodi ya juu ya kufuta ujinga Afrika kwa 90%. Mnamo Mwaka 2005 alitunukiwa shahada ya heshima ya Uprofesa na Chuo Kikuu cha Diplomasia huko China kwa uwezo wake wa kusomea karibu fani zote muhimu duniani ikiwemo sheria, uchumi, historia, sayansi, sanaa, utawala na elimu.......yasemekeana rafiki mkubwa wa maisha ya Mugabe ​tangu utotoni ​ ​​ni 'Kitabu kwa sana'​ ​.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...