Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli amemteua Profesa Mohamed Janabi (pichani) kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ( The Jakaya Kikwete Cardiac
Institute ) iliyoko katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar
es salaam.
Profesa Janabi, ambaye pia ni daktari Mkuu Binafsi wa Rais
Mstafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alikuwa akikaimu nafasi hiyo toka
kuanza rasmi kwa taasisi hiyo Septemba 2015 na inayoendelea kujizolea sifa kwa
huduma zake za moyo ambazo awali
zilipatikana nje ya nchi. Tasisi hiyo hivi sasa inajitegemea.
Taasisi ya Jakaya Kikwete inatoa matibabu pamoja na mafunzo ya Ubingwa wa juu katika fani ya
Upasuaji wa Moyo , Usingizi na Tiba ya Moyo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha
Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili( MUHAS) na taasisi za moyo mbalimbali duniani.
Hivi majuzi Chuo cha Magonjwa ya Moyo cha Marekani (American College of Cardiology) kimemteua Profesa Janabi kuwa mwanachama (Fellow of American College Cardiology) wa taasisi hiyo yenye wanachama mabingwa 52,000 dunia nzima, akiwa mtu wa kwanza nchini kutunukiwa FCC.
Taasisi hiyo ina matawi (Chapters) dunia nzima isipokuwa Afrika. Afrika Kusini wana mpango wa kufungua Chapter ambapo ili kuianzisha tawi wanahitajika wanachama sio chini ya 20.
Kwa mujibu wa Profesa Janabi, hapa Afrika Mashariki juhudi hizo zimeanza ila kwa sasa Kenya ina Fellows wanane na Tanzania ni mmoja pekee ambaye ni yeye Profesa Janabi. Wanahitaji fellows wengine 11 kutimiza idadi ya kuwa na tawi.
"Kuna faida nyingi sana kuwa kwenye taasisi hiyo katika kupata elimu ya magonjwa ya moyo, uwezeshaji rasilimali watu (capacity building) na kadhalika.
"Sisi tuna bahati kwani Makamu wa Rais wa ACC Profesa Mike Valentine kutoka Central Virginia Marekani aliwahi kuwa mwalimu wangu. Yeye alikuja hivi majuzi kwenye kongamanoi letu (2nd East Africa Cardiology Conference) na pia alianzisha mchakato wa wa kuanzisha chapter ya Afrika mashariki iwe hapa Tanzania kutokana na mafanikio yanayoendelea JKCI" Profesa Janabi, ambaye sasa ni Prof. Mohamed Janabi MD., MTH., PhD., FACC, ameiambia Globu ya Jamii.

Profesa Janabi ni
mmoja kati ya viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za serikali ambao waliteuliwa
kushika nyadhifa July 16, 2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli.
Wengine walioteuliwa ni Mhe. Augustino
Lyatonga Mrema ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya
Parole, Prof. William R. Mahalu aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Prof.
Angelo Mtitu Mapunda ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna
wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu
umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Wengine walioteuliwa ni
Sengiro Mulebya (Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama), Oliva
Joseph Mhaiki (Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu
(TSC), Winifrida Gaspar Rutaindurwa (Katibu wa Tume ya Utumishi wa
Walimu (TSC), Charles Rukiko Majinge (Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini
ya Hospitali ya Taifa Muhimbili) na Dkt.
Julius David Mwaiselage ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza
tarehe 15 Julai, 2016.
SAFI SANA ...
ReplyDelete