Na Selemani Semunyu JWTZ
Wanariadha wa Timu Teule ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ  imemuahidi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Davis Mwamunyange kurejesha heshima katika Michezo kwa kuleta medali nyingi kutoka Rwanda.
Hayo yamesemwa Mwishoni mwa Wiki na Wanariadha hao wakati walipotembelewa na Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa JWTZ Brigedia Jenerali Martin Busungu  katika kambi yiliyowekwa Katika eneo la Sanu Baray Wilayani Mbulu Mkoani Manyara.
Walisema  Maandalizi ya Safari hii kuelekea mashindano ya Afrika Mashariki yanayotarajia kufanyika Agosti Mwaka huu Nchini Rwanda ni Maandalizi ya kina ukizingatia Jeshi likiwa limewawezesha ipasavyo hivyo hawana sababu ya kukosa ushindi.
Mmoja wa Wanariadha hao ni Jackline Sakilo ambaye ni mmoja wa wanariadha tishio alisema kambi imewekwa katika eneo ambalo lina hali ya hewa inaruhusu ambayo ni Futi 1980 kutoka usawa wa bahari hivyo Mkuu wa majeshi ajiande kupokea medali kutoka kwa Vijana wake .
“ Mkuu wa majeshi ya Ulinzi lakini pia Rais na Amiri Jeshi Mkuu Afande Dk Magufuli wajiandae tu kupokea Medali kwa Niaba ya Watanzania  kwani ndio tunakwenda kuwawakilisha watuombee ili ndoto zetu zitimie” Alisema Jackline.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili Brigedia Jenerali Busungu amewataka Wanariadha hao kutunza Morali yao na mabadiliko ya Umbali isiwe kigezo cha Kufanya Vibaya kwani yametokea dakika za Mwisho na ni Kwa Nchi zote.
“Sasa Wanariadha wote watakimbia Kilometa 10 badala ya Kilometa Nane kwa wanawake na kilometa 12 kwa Wanaume kama ilivyozoeleka na kutangazwa Awali lakini kwa maandalizi haya ni matumaini yangu tutafanya vyema tu” Alisema Brigedia Jenerali Busungu.
Aliongeza kuwa Jeshi linamategemeo kwa Wachezaji wote wa Timu teule za Jeshi lakini pia Wananchi kwa ujumla wanategemea Timu yao itafanya vyema hivyo wanapaswa kupigana vilivyo kuibuka na ushindi kwa kila Mchezo.
Brigedia Jenerali Busungu aliongeza kuwa amesikia ahadi ya wachezaji ya kupata ushindi na kuleta medali nyingi na kuwapongeza kwa ahadi hiyo na kutaka sasa ikafanyike kwa vitendo.
Mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki yanatarajiwa kufanyika Kigali Nchini Rwanda kuanzia Agosti Saba hadi Agosti 17 Mwaka huu Nchini Rwanda huku Tanzania katika Riadha itapeleka Wanariadha 12 Wanawake Sita na Wanaume Sita.
 Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa JWTZ Brigedia Jenerali Martin Busungu akisalimiana na Mwanariadha Jackline Sakilo mara baada ya kutembelea katika kambi ya Timu Teule ya Riadha inayojiandaa na mashindano ya Afrika mashariki  iliyoko Mbulu Mkoani Manyara 
 Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa JWTZ Brigedia Jenerali Martin Busungu akizungumza na Wanariadha wanaojiandaa na mashindano ya Afrika Mashariki  alipowatembelea katika kambi ya Timu Teule ya Riadha  iliyoko Mbulu Mkoani Manyara 
 Wanariadha wa  Timu Teule ya JWTZ wakifanya mazoezi katika Kambi iliyoko Mbulu Mkoani Manyara ikiwa ni Sehemu ya Maandalizi mashindano ya Afrika mashariki yanayotarajiwa kufanyika Kigali Nchini Rwanda mapema Agosti Mwaka huu 
Wanariadha wa  Timu Teule ya JWTZ wakifanya mazoezi ya Viungo katika Kambi iliyoko Mbulu Mkoani Manyara ikiwa ni Sehemu ya Maandalizi mashindano ya Afrika mashariki yanayotarajiwa kufanyika Kigali Nchini Rwanda mapema Agosti Mwaka huu.
Picha zote na Selemani Semunyu wa JWTZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...