Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea ripoti ukaguzi wa asasi za kiraia kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Waziri wa Katiba na sharia Mhe. Amon Mpanju jijini Dar es Salaam. Serikali tayari imepanga kuzifuta Asasi za kiraia takribani 5,000 kutokana na Sababu Mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa asasi hizo usiofuata taratibu za Usajili.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bi. Emmy Kalomba Hudson akifafanua jambo akiwa na Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika mkutano wa kupokea ripoti ya ukaguzi kutoka kwa Taasisi zote zinazofanya usajili wa asasi za kiraia leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Waziri wa Katiba na sharia Mhe. Amon Mpanju.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...