Kwa mujibu wa familia marehemu Bi. Shakila Saidi anatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi Agosti 20, 2016 saa 10 alasiri katika makaburi ya Uwanja wa Ninja huko Mbagala Charambe jijini Dar es salaam
Namna ya kufika msibani nyumbani kwa marehemu kwa kutumia daladala. Unapanda magari ya Mbagala Rangi Tatu, ukifika mwisho unachukua basi la Nzasa na unashuka Mnara wa Voda hapo unauliza kwa Bi Shakila utaonyeshwa.
Bi Shakila alifariki jana baada ya kuanguka nyumbani kwake mara baada ya kuswali swala ya Magharibi. Kwa mujibu wa binti yake, Shani, mkongwe huyu wa taarabu hakuwa anaumwa wajati mauti yanamkuta.
KALALE PEMA PEPONI KIPENZI CHETU BI. SHAKILA
MOLA akulaze pema Peponi Kipenzi chetu Bi Shakila Saidi. Amen.
ReplyDeleteHivi hakuna picha ambazo aliwahi kujistiri mkaweka kaka michuzi eeh!
ReplyDeleteUmeuliza la maana mdau wa 2. Mini nadhani hawa wanahabari wetu wanahitaji mafunzo zaidi katika fani yao hiyo ya habari maana ni muhimu kujuwa picha ya aina gani inaendane na habari gani na mazingira gani, hilo bado ni tatizo, mana wanaweza kuweka picha ikamdhalilisha muhusika bila wao kujali.
ReplyDeletePumzika kwa amani Pema Peponi Daima Milele Bi Shakila Saidi. Amin.