Na Bashir Yakub.
Mara kadhaa linapoibuka suala la kugawana mali pale ndoa inapohesabika
kushindikana masuala kadhaa ya msingi na yanayohitaji uelewa huwa
yanaibuka.
Moja ya suala kati ya masuala ambayo huibuka ni hili la kutenganisha na
kufafanua hadhi ya mali za wanandoa ili mgawanyo uweze kufanyika kwa
haki. Yawezekana mwanandoa akadhani ana haki katika mali fulani lakini
kumbe kisheria hana haki hiyo ni mtazamo wake ndio unamsukuma kuamini
hivyo.
Halikadhalika yawezekana mwanandoa kudhani hana haki katika mali fulani
kumbe anayo haki. Ili kujua una haki ipi katika mali ipi na huna haki katika
mali ipi yahitajika kujua misingi ya kisheria inayotumika kugawanya mali za
wanandoa.
1.KUGAWANA MALI ZA WANANDOA.
Ieleweke kuwa tunapoongelea wanandoa kugawana mali tunaongelea talaka.
Hakuna kugawana mali bila talaka. Na kisheria talaka inapotoka tu swali
linalofuata ni habari ya mali na watoto kama wapo. Mali si lazima magari
na manyumba lakini pia hata vyombo vya ndani vikiwemo vitanda, makabati,
sahani n,k nazo ni mali kwa mujibu wa sheria. Navyo huhitaji mgao.
2. JE KUGAWANA MALI NI NUSU KWA NUSU ?.
Linapokuja suala la kugawana mali wengi hudhani mtindo unaotumika kugawa
ni ule wa nusu kwa nusu. Jambo hili si kweli kwakuwa sheria ya ndoa
1971 iliyofanyiwa marekebisho 2002 haisemi kuwa utaratibu wa kugawana
mali ni nusu kwa nusu. Sheria hii imeweka msingi mkuu wa kugawana mali
ambao ndio hutumika katika mahakama zetu katika kutoa maagizo ya
kugawa mali za wanandoa.
Msingi uliowekwa na sheria ni msingi wa kiwango cha mchango wa
mwanandoa katika kupatikana kwa mali husika. Kiwango alichochangia
mwanandoa katika kupatikana kwa mali hiyo ndicho kitakachokadiriwa na
kiwango hicho ndicho atakachopewa.
Kwa hiyo kama ni nyumba ya vyumba sita mmoja anaweza kupata chumba
kimoja na mwingine akapata vitano kutegemea na mchango wake. Na
mchango hapa sio leta ni lete. Mchango sio hela tu hata kazi za nyumbani
anazofanya mama wa nyumbani ambaye haleti hela nazo huitwa mchango
ambapo hukadiriwa na kupata kile anachostahili.
3. MALI KABLA YA NDOA NA BAADA YA NDOA.
Katika kutenganisha mali za wanandoa huwa zinatenganishwa katika
makundi makuu matatu. Kwanza kuna mali ambazo mtu alikuwa nazo kabla
ya ndoa na wakati anaingia katika ndoa ameingia nazo. Kwa mfano
mwanamke ameolewa akamkuta mwanaume tayari ana nyumba yake. Pili
kuna mali ambazo zimepatikama wakati wawili wakiwa katika ndoa .
Kwa mfano ndoa imefungwa wawili wakaanza kuishi pamoja na taratibu
wakaanza kujenga na kukamilisha. Na tatu ni mali ambazo zimepatikana
katika ndoa lakini zikiwa hazina uhusiano wowote wa kindoa kwa mfano
kurithi au kuzawadiwa mali. Tutaona hapa chini mazingatio ya sheria ya kila
moja katika haya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...