STARTIMES
imefanya Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga na Filamu za
Beijing ya mwaka 2016 kwa mara ya pili jijini Dar es Salaam kwa lengo
la kuendelea kukuza ushirikiano wa iutamaduni baina ya China na Tanzania.
Akizungumza
wakati wa maonyesho hayo yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency
Kilimanjaro jijini Dar es Salaam leo asubuhi, mgeni rasmi Naibu Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa
kwa muda mrefu serikali ya China na Tanzania zimekuwa na mahusiano
mazuri katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
“Mahusiano
mazuri ya kiutamaduni ndiyo yaliyopelekea serikali hizi mbili kuendelea
kushirikiana na kuwa marafiki mpaka hivi leo. Uhusiano huo si tu
unatunufaisha katika masuala ya kiuchumi bali pia kijamii. Kupitia
kazi za sanaa kam vile tamthiliya za michezo ya kuigiza na filamu watu
huweza kujua na kujifunza tamaduni za kila upande.
Nawapongeza
StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China nchini Tanzania kwa
kutuletea maonyesho haya ambayo nina hakika yatakuwa na manufaa makubwa
kwa tasnia yetu.” Alisema . Wambura
“Pia
ningependa kuwapongeza StarTimes kwa juhudi zao za dhati katika kukuza
utamaduni wetu kuipa nafasi lugha ya Kiswahili kuwa mojawapo inayotumika
kutafsiri filamu na tamthiliya hizi za michezo
ya kuigiza. Nimesikia mlifanya shindano la vipaji vya sauti ambapo
watanzania kumi walipatikana na watakwenda kufanya kazi katika makao
yenu makuu yaliyopo Beijing.
Hii ni hatua nzuri
na jambo la kuigwa kwa kukipa Kiswahili nafasi kubwa. Ninegependa
kumalizia kwa kutoa wito kwa washindi waliopatikana kwenda huko China
kutuwakilisha vema kama mabalozi wetu na kukifanya Kiswahili kiendelee kutambulika zaidi.” alisema Wambura
Akielezea
umuhimu wa maonyesho hayo Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,.
Guo ZiQi amebainisha kuwa kihistoria China imedumisha kwa dhati urafiki
na mataifa ya Afrika na kushirikisha tamaduni ndio njia madhubuti
itakayoenzi mahusiano hayo.
‘’Utofauti
ndio unaofanya dunia pawe mahala pazuri pa kuishi na China na Tanzania
kwa muda mrefu zimedumisha utamaduni wao unaovutia zaidi. Katika kilele
cha mkutano wa jukwaa la ushirikiano baina ya China na Afrika
uliofanyika mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya watu wa China,
Xi
Jinping alionesha nia ya kujizatiti katika kudumisha mahusiano mazuri
ya kiutamaduni, kuimarish mafunzo baina ya China na Afrika ili kusonga
mbele kwa pamoja na vilevile kuhakikisha mustakabali wa ukuaji wa
urafiki baina ya China na Afrika.’’Alisema ZiQi
‘’Kwa
kuendelea kukua kwa mahusiano ya maingiliano ya kiutamaduni baina ya
watu wa China na Waafrika, michezo ya kuigiza ya runinga na filamu za
Kichina imezidi kujizolea umaarufu na kuwa kichocheo muhimu katika
kujenga mahusiano baina ya pande hizo mbili. Kwa hivi sasa Beijing
inaongoza China katika uzalishaji wa michezo ya kuigiza ya runinga na
filamu.
Mpaka
hivi sasa ina taasisi takribani 3,400 zilizojikita katika uzalishaji wa
filamu na vipindi vya uninga na uendeshaji, vikiwa tayari
vimekwishazalisha zaidi ya mfululizo wa vipindi vya runinga 3,000 na
karibuni filamu 300 kwa mwaka.’’ alisema ZiQi
Washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano ya sauti waliopatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China wakionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Washiriki 10 walishinda mashindano hayo. Kutoka kushoto ni Hilda Malecela, Safiya Ahmed na Sadiq Kututwa.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akizungumza na washindi hao.
Washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka (kushoto) Muwakilishi wa Mamlaka ya Halmashauri ya Beijing, Yang Peili, Meneja Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa, Dk. Ayoub Riyoba, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, Muwakilishi wa Ubalozi wa China nchini, Guo HaoDong, Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes, Guo ZiQi na Kansela wa Utamaduni katika Ubalozi wa China nchini Tanzania, Gao Wei wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...