Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO),
limeendelea kufanya opresheni maalum ya kubaini wizi wa Maji kwenye maeneo ya
jiji la Dar es salaam na kubaini baadhi ya majengo ya kata ya kariakoo yakiwa
yamejiunganishia kinyume cha utaratibu.
Akizungumza katika operesheni hiyo maalum, kiongozi wa operesheni
kutoka ofisi ya Dawasco mkoa wa Ilala Bw. Gadimula Temba amesema kuwa wamebaini
wizi wa Maji kwenye jengo linalomilikiwa na ndugu Mahsen Mohamed ambapo alikuwa
amefungiwa laini ya Majisafi na amekuwa akidai hapati maji kila ifikapo kipindi
cha kusoma mita licha ya mita yake kusoma nakuonyesha kuwa ana deni la shilingi
laki tisa na ndipo walipokwenda mafundi kuchunguza nakubaini kuwa
amejiunganishia laini tatu za majisafi pamoja nakufunga mota yakuvuta maji
kwenye laini hizo zisizokuwa na mita.
“leo tumebaini wizi wa Maji kwenye jengo la ndugu Mahsen Mohamed
ambaye amekuwa akidai kuwa hapati Maji ya Dawasco kwa muda mrefu licha ya mita
yake kusoma nakuonyesha anadaiwa kiasi cha shilingi laki tisa ndipo tukaamua
kufanya uchunguzi nakubaini anatumia Maji yetu na pia amejiunganishia laini
tatu za maji zisizokuwa na mita pamoja nakufunga mota yakuvuta maji.
“Ila pia tumebaini kuwa amejiunganisha kwenye huduma ya mfumo wa
Majitaka kinyume cha utaratibu bila kibali kutoka Dawasco na amekuwa
akikataa kuwa hatumi mfumo wetu” alisema Temba.
Hata hivyo Dawasco imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kung’oa mota
ya kuvuta majisafi, kufunga laini zote za majisafi na ya majitaka pamoja na
kumtaka mmiliki wa jengo hilo kufika kwenye ofisi za Dawasco kwa taratibu
zingine za kisheria.
Nae afisa mtendaji wa kata ya Kariakoo Bw. Adeltus Kazinduki
amewataka wamiliki wa majengo makubwa kariakoo kuachana na tabia ya wizi wa
maji kwani ofisi yake kata inashirikiana na Dawasco mkoa wa Ilala kubaini watu
wote na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika.
“kwa kweli ofisi yangu ya kata ya kariakoo haitamvumilia mmliki
yoyote ambaye anafanya wizi wa Maji kwasababu sisi na Dawasco tumekaa kikao cha
pamoja nakukubaliana kuwa na ushirikiano hivyo mmiliki wa jengo lolote atakaye
kamatwa atachukuliwa hatua kali za kisheria” alisema Kazinduki.
Hata hivyo mmiliki wa jengo hilo Bw. Mahsen Mohammed hakuweza
kupatikana na hata wapangaji wa jengo hilo walidai hawajui makazi yake kwani ni
mtu wa kusafiri mara kwa mara .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...